Ewura yazindua ripoti ya utendaji kazi wa mamlaka za maji hapa nchini

 

Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa,akizungumza wakati wa Mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya tathmini
ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na vitabu vya mwongozo wa uaandaji
wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maji iliyozinduliwa leo Mei 11,2021
jijini Dodoma.



Waziri
wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ,akizungumza wakati wa Mkutano wa uzinduzi
ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji nchini
iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na
vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maj
iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.



Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje akitoa taarifa
kuhusu ripoti hiyo wakati wa uzinduzi ripoti ya tathmini ya utendaji
kazi kwa Mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa
Nishati na Maji (EWURA) na vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya
maji kwa Wizara ya Maj iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.



Baadhi
ya washiriki wa Mkutano wa Watendaji wa Sekta ya Maji
wakimsikiliza,Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati
wa uzinduzi wa ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji
nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA)
na vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maji
iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.



Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,akiangali
ripoti baada ya kukabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi
Godfrey Chibulunje (wa mwisho kutoka kushoto) mara baada ya kuzindua
ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji nchini
iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na
vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maji
iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.



Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,akimkabidhi hundi Mwenyekiti wa Bodi
Mhandisi Bashiri Mrinfoko wa tatu kushoto ( wa kwanza kushoto) ni
Mkurugenzi Mhandisi Mgeyekwa baada ya Moshi kuibuka Mshindi wa Jumla
wa Kwanza katika utendaji wa utoaji huduma yanmaji na usafi wa mazingira
katika kundi la mamlaka za Miradi ya Kitaifa
wakati wa uzinduzi ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za
maji nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji
(EWURA) na vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara
ya Maji iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.



Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,akimkabidhi hundi Mwenyekiti wa Bodi wa
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi Prof. Jafari Kideghesho
Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Moshi, Mhandisi Kija
Limbe baada ya Moshi kuibuka
Mshindi wa Jumla wa Kwanza katika utendaji wa utoaji huduma ya maji na
usafi wa mazingira katika kundi la mamlaka za maji za mikoa mara baada
uzinduzi ripoti ya tathmini ya utendaji kazi kwa Mamlaka za maji nchini
iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na
vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya maji kwa Wizara ya Maji
iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.



Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,akikabidhi hundi Mwakilishi wa Mamlaka ya
maji na usafi wa mazingira Biharamulo Bw.Mahmudu Bishanga kushoto kwake
ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Biharamulo mara
baada ya Biharamulo kuibuka mshindi wa kwanza katika utendaji wa utoaji
huduma ya maji na usafi wa mazingira katika kundi la mamlaka za maji za
Miradi ya kitaifa wakati wa uzinduzi ripoti ya tathmini ya utendaji
kazi kwa Mamlaka za maji nchini iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa
Nishati na Maji (EWURA) na vitabu vya mwongozo wa uaandaji wa miradi ya
maji kwa Wizara ya Maji iliyozinduliwa leo Mei 11,2021 jijini Dodoma.


……………………………………………………………………………….


Na.Alex Sonna,Dodoma


Mamlaka
ya udhibiti wa huduma za nishati na maji hapa nchini UWURA leo Mei 11,
2021 imezindua ripoti ya tathmini ya hali ya utendaji kazi na utoaji
huduma kwa mamlaka za maji hapa nchini ripoti inayolenga kuimarisha
utoaji wa huduma za maji kwa wananchi.


Akizindua
ripoti hiyo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa amewataka watendaji katika mamlaka zote za maji ngazi zote hapa
nchini kufanya kazi kwa kutanguliza uzalendo, uadilifu na weredi katika
kazi zao.


Amesema
Serikali imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha huduma ya maji
inawafikia wananchi kama inavyotakiwa lakini kuna baadhi ya watendaji
hawatimizi majukumu yao vizuri.


“Serikali
inatumia fedha nyingi sana katika kutekeleza miradi lakini miradi hiyo
haifanyi kazi kwa uzembe wa watendaji katika kusimamia miradi hiyo,
nataka kila mmoja afanye kazi kwa weredi mkubwa ili wananchi wapate
huduma za maji” amesema Mhe. Majaliwa.


Waziri
Mkuu Majaliwa pia amezitaka mamlaka za maji kwenda kusimamia ipasavyo
ukusanyaji wa ankara za maji ili kuwezesha mamlaka hizo kuendelea
kujiendesha bila hasara huku zikizingatia sheria bila kuwabambikizia
Ankara watumiaji wa maji kwani kuna malalamiko mengi sana.


Ameongeza
kuwa “mkahamasishe watu kulipa ankara za maji na h ii sio kwa wananchi
tu hata kwenye taasisi za serikali zote zilipe bili yeyote anayetumia
maji lazima alipe ankara za maji mkasimamie hilo, pia tumepiga marufuku
ukataji wa maji siku za wikendi au siku kuelekea wikendi” amesema.


Aidha
ameitaka EWURA kwenda kusimamia uboreshwaji wa huduma za maji na
kujenga utaratibu wa kufuatilia uboreshaji wa sera na kanuni katika
kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji ipasavyo na kufuatilia
tatizo la ucheleweshwaji wa miradi ya maji.


Awali,
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema wao kama Wizara watahakikisha
wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora
za maji na hawatamvumilia mtu yeyote atakayekwenda na kutaka kurudisha
nyuma jitihada hizo.


Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje
akitoa taarifa kuhusu ripoti hiyo amesema ripoti hiyo itasaidia katika
kuimarisha utendaji kazi kwa Mamlaka zote na watakuwa wakitoa ripoti ya
tathmini iliyofanyika ya utendaji wa kila Mamlaka katika mamlaka za
Mikoa na miradi ya kitaifa na mamlaka za miji midogo na Wilaya.


Amesema
wamefanya tathmini ya utendaji wa kila mamlaka na kupata Mamlaka
zilizofanya vizuri katika kutoa huduma katika makundi ambapo kwa kundi
la usimamizi wa miradi ya kitaifa aliyeibuka mshindi ni KASHWASA,
Mamlaka za Mikoa ni Mamlaka ya Mkoa wa Moshi na Mamlaka za miji na
Wilaya ni Bihalamuro ambazo zimezawadiwa shilingi milioni 21 kila mmoja
ambazo watazitumia katika kununua dira za maji.