Fursa nyingi za kilimo cha umwagiliaji kupatikana madaba

 


Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Madaba Bw. Mikael Hadu, na wataalam kutoka katika Halmashauri hiyo na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao Mapema leo Wilayani Madaba.
Mchumi kutoka Halmashauri ya Madaba Bw. Bosco Mwingira akiwasilisha
jambo wakati wa kikao hicho na Kulia ni Bw. Yassin Kazoba  mchumi kutoka
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Picha ikionesha baadhi ya  wakulima wanawake wa Skimu ya
Kilimo cha umwagiliaji cha HangaNyadinda katika kikao na wataalam
kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
Mwenyekiti wa Skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji ya HangaNyadinda Bw.John
Joakim Komba akifafanua jambo kwa wakulima wakati wa kikao na wataalam
kijijini hapo.

Na Mwandishi wetu–
MADABA

IMEELEZWA kuwepo kwa fursa nyingi za kilimo cha
umwagiliaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma, kutokana na kuwepo
kwa eneo kubwa lenye mabonde yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji licha ya maeneo
hayo kutoendelezwa.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Madaba Bw.Mikaeli Hadu, alipokuwa akizungumza na wataalam kutoka
Tumeya Taifa ya Umwagiliaji waliyopo katika ziara ya kikazi ya kutoa elimu na mafunzo
katika baadhi ya skimu za wilaya hiyo  wakianzia
na skimu ya Hanga  Nyadinda.

“Kuna fursa nyingi sana za kilimo hiki
cha Umwagiliaji katika mkoa huu hasa kwa upande huu wa kuelekea Njombe, kwani mapori
yanayofaa kwa kilimo ni mengi na wananchi wa maeneo haya ni wakulima wachapa kazi
hivyo, Idara ya Umwagiliaji itakapokuwa katika zoezi la kuongeza eneo la
Umwagiliaji ni vizuri ikaangalia maeneo haya katika jicho la kipekee na kuyaboresha,
kwani wananchi wengi wamekuwa wakilima kienyeji, yaani kilimo cha vinyungu katika mabonde mengi hivyo eneo likiongezwa
litahamasisha zaidi kilimo cha umwagiliaji.” Alisema.

Bw. Hadu aliendelea  kusema kuwa zipo skimu ambazo serikali imewekeza
kwa ajili ya   umwagiliaji lakin iwananchi
hawa zitumii vizuri kitolea mfano wa skimu ya mbanga mawe, “Serikalii na  tililia mkazo kilimo cha umwagiliaji ihivyo kuna
kila sababu ya skimu hizi kufanya vizuri, wakulima wahamasishwe vya kutosha nakupewa
elimuili uwekezaji huua mbao serikali imewekeza pesa nyingi ufanye kazi kwani utaboresha maisha ya wananchi.” Alisisitiza.

Akiongelea swala la migogoro kati ya wakulima
na wafugaji wilayani Madaba, Bw. Hadu alisema mkoawa Ruvuma umekuwa na uingiaji
mkubwa sana wa mifugo kutoka mkoa wa Mwanza, Simiyu na Rukwa na Halmashauri hii
ndiyo lango kubwa sana la kupitisha Mifugo.

 “Tumekuwa wakali sana kuhakikisha kuwa mifugo inayoingia
ni yakuchinjwa na siyo ya kufuga lakini wafugaji ni wajanja wanachukua vibali kwa
ajili ya kuleta ng’ombe wa kuchinja lakini wao wakiingia wanafuga, kwa hiyo tunaendelea
saana kufuatilia jambo hili kwakushirikiana na Idara ya Mifugo ilikuweza kutatua
migogoro inayojitokeza baina ya  wakulimana
wafugaji iliwote,wasipate madhara.” Alibainisha.

Halmashauri ya wilaya ya Madaba ina skimu
nne za kilimo cha umwagiliaji ambazo ni Luhimba, Ngadinda, Mbangamawe na Gumbiro
zinazotajwa kuhitaji zaidi elimu kwa wakulima ambapo wataalam wakilimo cha
umwagiliji walipata fursa ya kutoa elimu kuhusu Sheria ya Taifa ya Kilimo cha
umwagiliaji na Mfuko wa maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji katika skimu ya Hanga
Nyadinda..