Mbunge wa Jimbo la Arusha,Mrisho Gambo, Desemba amekabidhi msaada wa Visaidizi mwendo100, kwa watu wenye changamoto ya viungo vya mwili ikiwa ni kutekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu Oktoba mwaka 2020.
Akikabidhi awamu ya kwanza ya visaidizi hivyo,Gambo,amesema kabla alifanya sense katika kata zote 25 na kugundua kuwa kuna watu 500 wenye changamoto za viungo wanaohitaji visaidizi mwendo.
Amesema kuwa visaidizi mwendo hivyo vimetolewa kwa kushirikiana na shirika la kuhudumia walemavu nchini CCRBT,na vimetolewa kwa watu wote kuanzia umri wa miaka miwili hadi watu wazima ambao wanakabiliwa na changamoto ya kufika eneo moja kwa wakati.
Aidha amesema mwezi Januari au Februari mwaka 2021 atawaunganisha walemavu wote wasiokuwa na uwezo kwenye mfuko wa bima ya afya NHIF, ili waweze kupata matibabu kwenye hospitali mbalimbali nchini .
Tayari Mbunge huyo katika kutekeleza ahadi zake ameshachimba kisima kirefu cha maji ndani ya soko la Kilombero ili kuwaondolea usumbufu wafanyabiashara ndani ya soko hilo, na ameahidi kuchimba visima kwene soko la Samunge,soko la Kijenge na soko kuu .
Mapema mwezi Novemba mwaka 2020, mbunge huyo ameshakabidhi vifaa vya ujenzi (nondo roli moja na Saruji) kwa shule ya sekondari kata ya Ungalimited ,ambayo itakuwa ni jengo la ghorofa nne.