Hatimaye jwtz kukarabati barabara ndani ya mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro

Na Ahmed Mahmoud,Arusha
Baada ya
taarifa za kusambaa kwa picha zinazoonesha ubovu wa miundombinu ya
barabara katika eneo la kitalii la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
lililopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha,mamlaka hiyo imetangaza
kuzifunga baadhi ya barabara zinazokwenda katika eneo hilo.
Kwa
muktadha huo ili kuzifanyia ukarabati wa kina ili ziweze kupitika na
kuondoa sintofahamu ya miundombinu ya barabara  kutokana na uharibifu
uliofanywa na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini hivyo kuchukuwa
hatua za haraka kudhibiti kadhia hiyo.
 Baada
ya kusambaa kwa picha hizo mkuu wa mkoa wa Arusha aliliagiza jeshi la
polisi kuwatafuta na kuwakamata wale waliosambaza picha hizo kwa madai
ya kuhujumu uchumi.
 Juhudi
hizo za ukarabati wa miundombinu ya barabara za mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro ni moja ya kuongeza suala zima la ubora utakaosaidia wageni
wanaotembelea hifadhi hiyo kufika kwenye maeneo yote ya vivutio vya
mamlaka hiyo ya hifadhi.
Akiwa
katika  Kreta ya Ngorongoro, miongoni mwa vivutio vya kitalii vilivyopo
katika hifadhi hiyo, mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro Profesa Abiud Kasomila amewaambia waandishi wa habari kuwa
jeshi la wananchi Tanzania JWTZ ndio watakaohusika kutengeneza
miundombinu hiyo.
Alisema
kuwa Jeshi la wananchi wa Tanzania ndio wataendelea na matengenezo ya
barabara kutokana na wao kuwa na uzoefu mkubwa wa masuala hayo na hivyo
baadhi ya barabara zitafungwa mpaka pale marekebisho yatakapokamilika.
Hifadhi
ya Ngorongoro ina eneo lenye ukubwa wa kilometa 8,300 za mraba lenye
mchanganyiko wa aina yake wa sura ya nchi, wanyamapori, wanyama wafugwao
na mambo ya kale.
Hifadhi
hiyo ni miongoni mwa hifadhi zilizo na vivutio vya kipekee vya kitalii
duniani kutokana na kuwa na maeneo maarufu kama vile bonde la Olduvai
Gorge ambapo inaaminika fuvu la binadamu wa kwanza lilipatikana hapo.
Ngorongoro
Kreta, pamoja na kujumuisha maisha mseto ya wanyama na binadamu,kwa
umuhimu huo basi mamlaka ya hifadhi hiyo imeona ni vyema kufunga baadhi
ya barabara ili kushughulikia changamoto hizo.
Dkt.Fred
Manongi ni kamishina wa mamlaka ya hifadhi hiyoanataja baadhi ya maeneo
ya kitalii yatakayofungwa ikiwemo barabara ya kwenda eneo la kreta na
maeneo ya Laitol ambayo yamekuwa na changamoto kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha.
Sakata
hili lilianzia katika mitandao ya kijamii baada ya kusambaa kwa picha
zinazoonesha miundombinu ya barabara kuharibika vibaya kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha.
 Licha
ya maagizo ya serikali ya mkoa wa Arusha ya kuwakamata wote waliohusika
kusambaza picha hizo,  baadhi ya waongoza watalii wameipongeza mamlaka
ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kushughulikia suala hilo.
Alisema
kuwa changamoto hiyo inaendelea kufanyiwa kazi na watahakikisha
wanakamilisha ndani ya muda kuondoa hali hiyo ili wageni waendelee
kupata huduma za utalii maeneo yote ya he hifadhi hiyo.