Hukumu ya rais wa zamani wa tff jamal malinzi na wenzake kusomwa disemba 5 mwaka huu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema itatoa hukumu dhidi ya Rais wa zamani wa TFF Jamal Malinzi na wenzake watatu Desemba 05 mwaka huu.


Malinzi, Mwesigwa, Mwanga na Flora wanakabiliwa
mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia
ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha Dola za Kimarekani 173,335.

Hukumu
hiyo ilipangwa kusomwa jana lakini Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi,
alisema bado haijakamilika na kwamba itasomwa tarehe iliyopangwa.

Kesi hiyo imesikilizwa na Hakimu Mkazi Maira Kasonde lakini kwa sasa amehamishwa kituo cha kazi

Wakili
wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa
kwa ajili ya kusikiliza hukumu na upande wa Jamhuri ulikuwa tayari.

Hata hivyo, Hakimu Shaidi alisema hukumu ya kesi hiyo itasomwa Desemba 5, mwaka huu na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu