Jeshi la polisi mkoa wa shinyanga laendelea na misako kubaini wahalifu, vitu na vielelezo mbalimbali vya kamatwa

Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga limeendelea na misako ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita limekamata
vitu na vielelezo mbalimbali ikiwemo Bangi pamoja na pikipiki za wizi.

Hayo yamebainishwa na
kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa polisi Janeth
Magomi ambapo amesema jeshi hilo limeendelea kufanya doria na misako katika
maeneo mbalimbali sanjari  na kutoa elimu
kwa wananchi kupitia vyombo vya habari ili kuwajengea uelewa juu ya uhalifu.

Amesema jumla ya maderewa
6499 wa vyombo vya moto wametozwa faini ya makosa mbalimbali, wakiwemo madereva
6 wa magari wamepelewa mahakamani huku madereva watatu wakifungiwa leseni zao.

“Jumla
ya madereva 6 wa magari walipelekwa mahakamini kwa makosa ya usalama
barabarani, madereva 6499 wa vyombo vya moto walitozwa faini na pia madereva 3
walifungiwa leseni zao kwa upande wa mahakama jumla ya kesi 19 ziliweza
kufanikiwa ambapo kesi 3 za makosa ya kubaka zilihukumiwa kifungo cha kati ya
Miaka 30 hadi hadi kifungo cha maisha”.
amesema Kamanda Magomi

Kamanda Magomi ametaja
makosa mengine ya kesi mbalimbali zilizohukumiwa jela huku akitoa wito kwa
wananchi kuendelea kufuata sheria za Nchi na kutojihusisha na vitendo vya
kihalifu.

“Lakini
pia kesi moja ya kulawiti ilihukumiwa kifungo cha maisha jela, kesi moja ya
shambulio la aibu ilihukumiwa kifungo cha Miaka 20 jela na fidia ya shilingi
Milioni moja, kesi tatu za wizi zilihukumiwa kifungo cha Mwaka mmoja jela, kesi
moja ya ukatili dhidi ya mototo ilihukumiwa kifungo cha Miaka 3 jela pamoja na
faini ya shilingi laki tano pia kesi moja ya kumtorosha mwanafunzi ilihukumiwa
kifungo cha miaka 30 jela”.
amesema Kamanda Magomi

“Vile
vile kesi moja ya kughushi nyaraka ilihukumiwa kifungo cha miaka 5 jela, kesi
moja ya wizi wa mototo ilihukumiwa kifungo cha miaka 3 jela, kesi 2 za wizi wa
mifugo zilihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja hadi 5 jela na pia kesi mbili za
kujeruhi zilihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja hadi 5 jela kezi zingine mbili za
pikipiki zilihukimiwa kifungo cha miaka 2 
jela na nyingine ya wizi ilihukumiwa kifungo cha miaka 6 jela na kulipa
fidia ya shilingi milioni nane na kesi moja ya kupatikana na Bangi ilihukumiwa
miaka miwili jela”.
amesema Kamanda Magomi

“Tulifanikiwa
kukamata jumla ya gramu 2205 pamoja na kete 61 za dawa za kulevya aina ya Bangi,
pia tulikamata pikipiki 11, mifuko 24 ya cementi, ndoo 4 na makopo 4 ya rangi
za nyumba, tulikamata Gypsum powder na vifaa mbalimbali vya ramli chonganishi”.

“Pia
kutokana na ushirikiano mwema kati ya Polisi na jamii wananchi waliweza kutoa
taarifa za uwepo wa aina ya silaha aina ya Pistol browning ikiwa na risasi 12 silaha
hiyo iliweza kutelekezwa kwenye shule ya sekondari hapa Manispaa ya Shinyanga mtu
aliitelekeza chooni mpaka sasa bado hatujampata mmiliki wake”.
amesema
Kamanda Magomi

Kuelekea sikukuu za
krismas na mwaka mpya Jeshi la pilisI Mkoa wa Shinyanga limeendelea kujiweka
katika hali ya utayari ili kukabiliana na vitendo mbalimbali vya kihalifu na
kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.

Kamanda wa jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa polisi Janeth Magomi akitoa
taarifa ya mananikio kwa waandishi wa habari katika misako na doria
iliyofanyika kwa kipindi cha Mwezi mmoja.