Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa manyara laendelea kuusaka mwili wa mtoto aliyesombwa na maji kwa siku tatu sasa

Na John Walter-Babati
Mwili
wa Mwanafunzi wa kiume (10) aliekuwa akisoma darasa la nne katika shule
ya Msingi Darajani iliopo Mjini Babati mkoani Manyara  anaesadikiwa
kusombwa na maji wakati akiogelea kwenye mto eneo linalojulikana kama 
Darajani  unaotiririsha Maji kuelekea Ziwa Manyara bado haujapatikana
kwa siku ya tatu sasa.

Kamanda
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara, Kamishna msaidizi
Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Julishaeli Mfinanga,
amewataka wananchi wawe watulivu katika kipindi wanachoendelea na
utafutaji.

Amesema
mwelekeo wa kumpata mtoto huyo upo kwa sababu tabia ya maji huwa baada
ya mtu kuzama kwenye kina kirefu cha  maji baada ya siku tatu humuibua
juu na kumtupa kando ya mto.

Wananchi
kutoka maeneo mbalimbali ya mji wa Babati,Viongozi wa serikali na Siasa
wamejitokeza kwa wingi kusaidiana na vyombo vya ulinzi na Usalama
katika kufanikisha zoezi la kuupata mwili wa mtoto huyo.

Hata
hivyo  baaadhi ya wananchi wakizungumza na kituo hiki, wamesema kuwa
kwa kipindi hiki cha mvua mto huu huwa unafurika maji mengi ambayo yana
kasi kubwa, hivyo tahadhari inahitajika kwa wanaovuka katika eneo la mto
huo pamoja na kuwa makini na watoto.

Mtoto
huyo alisombwa na maji jumatatu Januari 20  majira ya saa saba mchana
wakati wakiwa wanaogelea yeye na wenzake ambao walinusurika.