Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika ametangaza kutogombea nafasi ya ubunge katika jimbo katika uchaguzi mkuu 2010 na badala yake amejipanga kutumikia nafasi ya Katibu Mkuu wa Chadema.
Kupitia ujumbe wake aliouweka kwenye mtandao wa twiter, mnyika ambaye anaonekana kufuata nyayo za aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA Dkt Slaa, aliyehamia CCM wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015, ambaye aliacha kugombea ubunge wa Karatu baada ya kuteuliwa kuwa Katibu mkuu wa chama hicho.
Katika ujumbe wake Mnyika amesema kuwa hata muasisi wa Tanzania hayati Mwalimu Nyerere aliamua kuachia uwaziri Mkuu na kuimarisha TANU hivyo na yeye anafuata nyayo hizo kutogombea tena ubunge na kujikita kwenye chama.