Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Magufuli amemteua Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina
Mwaimu kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Mwaimu kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi
imeeleza kuwa sambamba na uteuzi wa Mwenyekiti, Rais Magufuli amemteua
Mohamed Khamis Hamad (Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar) kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Pamoja na uteuzi huo, Rais Magufuli ameteua Makamishna wa Tume hiyo kama ifuatavyo;
Dkt. Fatma Rashid Khalfan. (Mhadhiriwa Chuo Kikuu cha Zanzibar).
Thomas Masanja (MhadhiriwaSheria, Chuo Kikuu cha MtakatifuAgustino – SAUT).
AminaTalib Ali (Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar).
Khatib Mwinyi Chande (Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu Huria Tanzania – OUT)
Nyanda Josiah Shughuli (Afisa Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango).
Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Septemba, 2019