Rc makonda apambana kutimiza maagizo ya rais magufuli

Ikiwa
ni siku kadhaa zimepita tangu Rais Magufuli, kutoridhishwa na
utekelezwaji wa baadhi ya miradi ya Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwemo
machinjio ya Vingunguti, Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda amelazimika 
kushiriki katika ujenzi wa machinjio hayo hadi nyakati za usiku ili
kuhakikisha miradi hiyo inakamilika.







Usiku
wa kuamkia leo Septemba 22,2019 RC Makonda  aliamua kwenda ‘site’ usiku
kushirikiana na Makandarasi waliopewa tenda ya ujenzi wa machinjio hayo
ya kisasa, ambapo amesema sauti ya Rais Magufuli kuhusu ujenzi huo,
imekuwa ikimfuata mara kwa mara hivyo ameona si vyema kumuangusha.




“Nimeamua
kusimamia mwenyewe sababu moja tu niliowaamini nakuwaachia kazi hii
wameniangusha na ile sauti ya Rais Magufuli, kuwa nimekubali hii miradi
ishindikane, isitekelezeke?, nakuambia Rais na Watanzania wote miradi
hii ntaisimamia mwenyewe usiku na mchana ili kuhakikisha ndoto uliyonayo
katika mkoa wetu inatimia, sitakuangusha” amesema Makonda.




Makonda amesema kwa sasa hatokuwa akipatikana ofisini, badala yake atakuwa akipatikana ‘site’ hadi miradi hiyo itakapokamilika.





Machinjio hayo yanatarajiwa kukamilika katika kipindi cha ya miezi 3 ijayo.