Kamati ya fedha na utawala pamoja na mkurugenzi wa manispaa ya shinyanga wafanya ziara kukagua miradi.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi
wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze leo Jumamosi Julai 22,2023 wamefanya
ziara kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa
katika Manispaa ya Shinyanga.

Miradi iliyotembelewa ni ujenzi katika shule ya sekondari
Old Shinyanga, ujenzi wa shule ya wasichana Butengwa kata ya Ndembezi, ujenzi
wa madarasa shule ya msingi mpya Ibadakuli, ujenzi wa jengo la wagonjwa wa
dharura (EMD) Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga pamoja na ujenzi wa jengo la
utawala Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza baada ya ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati
ya fedha na utawala ambaye pia ni Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias
Ramadhan Masumbuko amepongeza kwa hatua nzuri iliyofikiwa katika utekelezaji wa
miradi hiyo.

Mwenyekiti huyo amesema kamati imefurahishwa na hatua
iliyifikiwa katika miradi hiyo ambapo ameahidi kuendelea kusimamia mipango
iliyokusudiwa na serikali kupitia ilani ya chama cha mapinduzi CCM.

Mhe. Masumbuko ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi ya maendeleo Manispaa ya Shinyanga kupitia sekta mbalimbali ikiwemo
Afya, Elimu pamoja na sekta ya Maji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu
Alexius Kagunze serikali itaendelea kuweka msukumo katika miradi inayoendelea
ili iweze kukamilika kwa wakati.

Mkurugenzi Mwalimu Kagunze amesema miradi yote
inayotekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga imelenga kutatua changamoto
zilizopo pamoja na kuchochea uchumi kwa wananchi, Halmashauri na Taifa kwa
ujumla.

Mwalimu Kagunze naye amempongeza na kumshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutoa
fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya
Shinyanga huku akiahidi kusimamia vyema miradi yote ya maendeleo.

Amewata mafundi kuongeza kasi kwenye ujenzi ili miradi
hiyo iweze kukamilika kwa wakati ambapo amesema ataendelea kutoa ushirikiano
katika utatuzi wa changamoto zilizopo.

Kaimu wa Division ya miundombinu na maendeleo ya miji
na vijiji Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Kassim Thadeo  ameahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na
kamati ya fedha na utawala kwenye miradi ya maendeleo kutekelezwa.

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi
wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze leo wamefanya ziara kutembelea
na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wakiambatana na wataalam mbalimbali
wa  Manispaa ya Shinyanga.

Muonekano wa hatua zilizofikiwa za ujenzi katika shule ya sekondari
Old Shinyanga.

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi
wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze wakiwa katika zoezi la kukagua
ujenzi katika shule ya sekondari Old Shinyanga leo Jumamosi Julai 22,2023

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze wakiwa katika zoezi la kukagua ujenzi kwenye shule ya sekondari Old Shinyanga leo Jumamosi Julai 22,2023

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze wakiwa katika zoezi la kukagua ujenzi kwenye shule ya wasichana Butengwa kata ya Ndembezi  leo Jumamosi Julai 22,2023

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze wakiwa katika zoezi la kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura (EMD) Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga  leo Jumamosi Julai 22,2023

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze wakiwa katika zoezi la kukagua ujenzi wa shule ya msingi mpya Ibadakuli leo Jumamosi Julai 22,2023

Viongozi wakipokea taarifa.

Muonekano madarasa katika shule ya msingi Ibadakuli.

Kamati ya fedha na utawala kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze wakiwa katika zoezi la kukagua ujenzi wa jengo la utawala Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Julai 22,2023