Kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi wilaya wilaya ya shinyanga mjini yatoa msaada kitoa cha watoto wenye ulemavu.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kamati ya utekelezaji jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi CCM
Wilaya ya Shinyanga Mjini imetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa
watoto wenye ulemavu wa akili na viungo wanaolelewa katika Kituo cha Brothers
of Charity kilichopo kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Msaada huo ni pamoja na Mchele, Maharage, unga wa sembe, mafuta ya
kupikia, chumvi, juisi, biskuti na Sabuni na kwamba hatua hiyo  ni sehemu ya ziara ya kamati ya utekelezaji
Wilaya ya Shinyanga mjini leo Mei 12,2023 kabla ya kutembelea na kukagua uhai
wa jumuiya katika kaya ya Kitangili.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vyakula hivyo Mwenyekiti  wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga
mjini Bwana  Fue Mrindoko amesema jumuiya
hiyo imeguswa na changamoto zilizopo katika kituo hicho huku akiwaomba
wanachama, jumuiya zingine na wadau  mbalimbali
kuwa na utamaduni wa kusaidia wetu wenye uhitaji.

 “Jumuiya
ya Wazazi tunaendelea kutembelea kata mbalimbali kwa ajili kukagua uhai wa
Jumuiya, kuingiza wanachama wapya na kuhamasisha kuanzisha miradi ya kiuchumi
na tumekuja hapa kuwatembelea watoto wetu na kuwapatia hiki kidogo tulichokuja
nacho na tunaahidi kuendelea kufika hapa na tunaomba wadau wengine na wananchi
wajitokeze kusaidia watoto hawa ili kupunguza changamoto”,
amesema
Mwenyekiti Mrindoko.

“Tunawapongeza sana  walezi wa watoto hawa hii kazi mnayofanya
kulea na kuwafundisha watoto hawa mambo mbalimbali kwakweli kazi hii mnayofanya
ni kazi ya kubwa mno tunawashukuru na tunawapongeza sana  nimeambiwa watoto hawa walikuwa hawajui
chochote lakini mmewafundisha jinsi ya kujitambua na sasa wanafanya wao wenyewe
mbarikiwe  sana nasi tunaendelea
kukitangaza kituo hiki lakini pia tutaendelea kufika hapa ili tushirikiane
kutatua changamoto zilizopo”
,amesema Mwenyekiti Bwana
Mrindoko

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM Wilaya
ya Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi ametaja msaada huo kuwa ni
pamoja na Mchele, unga wa sembe, Maharage, mafuta ya kupikia, chumvi, juisi,
biskuti na Sabuni ambapo amesema jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na kituo
hicho katika kupunguza au kumaliza kabisa changamoto.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo cha Brother of Charity,
Brother George Paul Rice amesema kituo hicho kina zaidi ya watoto 20 na kwamba ameishukuru
jumuiya ya wazazi pamoja na kamati yake ya utekelezaji kwa kutoa msaada huo ambao
 utasaidia kupunguza changamoto ya
chakula kwa watoto wenye ulemavu wa akili na viungo.

Kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini
leo imetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto wenye ulemavu
wa akili na viungo katika kituo cha Brothers of Charity kilichopo mtaa wa
Majengo Mapya kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM
Wilaya ya Shinyanga mjini, Bwana Fue Mrindoko  akizungumza kwenye kituo
cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili na viungo cha Brother of Charity kilichopo
mtaa wa Majengo mapya kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Mei
12,2023.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM
Wilaya ya Shinyanga mjini, Bwana Fue Mrindoko  upande wa kushoto akizungumza kabla ya kukabidhi msaada kwenye kituo
cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili na viungo cha Brother of Charity kilichopo
mtaa wa Majengo mapya kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Mei
12,2023

  



Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya
Shinyanga Mjini, Bi. Doris Yotham Kibabi 
akizungumza kabla ya kukabidhi
msaada kwenye kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili na viungo cha
Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa
Mei 12,2023.

Mkurugenzi wa Kituo cha Brother of Charity,
Brother George Paul Rice 
akizungumza kwenye zoezi la Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga
Mjini kukabidhi msaada kwenye kituo hicho 
leo Ijumaa Mei
12,2023.

Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo cha Brother of
Charity, Brother Francis Bega 
kizungumza kwenye zoezi la jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya
Shinyanga mjini kukabidhi msaada leo Ijumaa Mei 12,2023.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya
Shinyanga mjini, Fue Mrindoko (aliyevaa kofia kushoto) na viongozi mbalimbali
wakikabidhi chakula
 katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili
na viongo cha Brother of Charity kilichopo Kata ya Kitangili Manispaa ya
Shinyanga