Na Veronica Kazimoto
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imewafikia na kuwaelimisha wafanyabiashara
zaidi ya 700 kupitia kampeni ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
iliyofanyika mkoani Morogoro.

Lengo la kampeni hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali
ya kodi pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa
wafanyabiashara hao.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki,
Afisa Msimamizi wa Kodi Mkuu wa TRA, Julius Mjenga amesema kuwa,
mamlaka hiyo ililenga kuwafikia wafanyabiasha 500 lakini kutokana na
mwitikio mkubwa, TRA imefanikiwa kuvuka lengo hilo na kuwafikia zaidi ya
700.

“Wiki hii moja ya elimu kwa mlipakodi, tuliwalenga wafanyabiashara wa
wilayani ambapo kumekuwa na changamoto ya kutokupata elimu ya kodi kwa
wakati. Nashukuru tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu tumeweza
kuwaelimisha wafanyabiashara 774 katika kampeni hii”, alisema Mjenga.

Mjenga ameongeza kuwa “Tumefika karibu wilaya zote za mkoa huu wa
Morogoro ambazo ni Malinyi, Ulanga, Kilosa, Mvomero, Kilombero na Gairo
na kila mahali tulipopita tumepata mwitikio mkubwa kutoka kwa
wafanyabiashara na wananchi mbalimbali.”

Kwa upande wa wafanyabiashara waliotembelewa na TRA, wameishukuru
mamlaka hiyo kwa kuwaelimisha masuala mbalimbali yanayohusu kodi na
kuomba elimu hiyo iwe endelevu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema
kuwa, TRA ya sasa sio ile ya zamani kwa sababu sasa hivi maafisa wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania wamekuwa karibu na walipakodi na siku hizi
hawana tabia ya kufunga biashara zao.

“Zamani mtu alikuwa akisikia watu wa TRA wanakuja, anafunga duka
anaondoka lakini siku hizi, TRA wamekuwa marafiki, wanatuelimisha na
wala hawafungi biashara zetu, kwakweli tunashukuru sana,” alisema
Eleonora Kisimba, mfanyabiashara wa duka la nguo wa wilayani Mvomero.

Naye Stanphord Mjumbe ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya
ujenzi wilayani Gairo mkoani hapa alisema kuwa, kampeni ya elimu kwa
mlipakodi ifanyike mara kwa mara kwa sababu wafanyabiashara walio wengi
hususani wadogo hawajasoma hivyo wanahitaji kuelimishwa zaidi juu ya
haki na wajibu wao katika ulipaji kodi.

“Sisi wafanyabiashara wadogo, tulio wengi hatujasoma hivyo tunahitaji
elimu hii angalau kwa mwaka mara tatu ili tuweze kuelewa kwa kina haya
mambo ya ulipaji kodi maana wakati mwingine tunakuwa hatujui haki zetu,”
alisisitiza Mjumbe.

Aidha, wafanyabiashara hao wameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania
kurejesha Kodi ya Zuio kwa wamiliki wa majengo kwa kuwa baadhi yao
hawataki wapangaji kuzuia asimilia kumi na kuiwasilisha TRA.

Vilevile, wameomba kuelimishwa jinsi ya kulipa kodi ya mapato kwa awamu
mara tu wanapokadiriwa kodi hususani kwa wafanyabiashara wapya kwani
wengi wao wanapitiliza tarehe za kulipa kodi hiyo kwa kukosa uelewa.

Kampeni ya huduma na elimu kwa mlipakodi imemalizika tarehe 17 Novemba,
2019 na ilifanyika katika Mikoa ya Morogoro na Pwani ambapo
wafanyabiashara wamepata fursa ya kutembelewa katika maduka yao na
wengine walihudhuria semina kwa ajili ya kuelimishwa masuala mbalimbali
yanayohusu kodi.