Kanisa la mfalme zumaridi ‘anayejiita mungu wa dunia’ lafungwa jijini mwanza

Uongozi wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza umepiga marufuku ibada zinazoendeshwa na kiongozi wa kanisa la Mfalme Zumaridi lililoko mtaa wa Iseni kata ya Butimba hadi hapo Serikali itakapojiridhisha kuwa ibada hazikinzani na sheria za nchi.

Agizo la kupiga marufuku limetolewa  jana Novemba 18, 2019 na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Daktari Philis Nyimbi akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo katika eneo la kanisa hilo.

Amesema
kanisa hilo limekuwa likitumia katiba ya kanisa lingine ambalo ni
Pentecoste Christian Church of Tanzania  na pia limekuwa likitembea na
Katiba ya Kanisa hilo.


DC Nyimbi amesema kiongozi wa Kanisa
hilo la Mfalme Zumarid amekuwa akiendesha kanisa hilo bila kufuata
sheria za nchi wala maandiko matakatifu kwa kujiita Mungu wa Dunia,
Mfalme wakati yeye ni Mwanamke.