Kauli ya humphrey polepole baada ya sumaye kung’oka chadema

Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole
amemwambia Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye kuwa alimueleza
asingeweza kupata kazi ya kushauri chama chochote cha siasa kama
angekuwa nje ya Chama Cha Mapinduzi.


Polepole
ametoa kauli hiyo saa chache baada ya Waziri Mkuu Mstaafu Frederick
Sumaye kutangaza kujiondoa ndani ya CHADEMA kwa kile alichokidai kuwa
hakuna demokrasia ya kweli.

Polepole
ameandika; Mzee nilikwambia, kazi ya ushauri hutaipata ukiwa nje ya CCM
wenzako wanaotushauri na tunazingatia ushauri wao kwasababu
tunawaheshimu, ni wana CCM na kiitikadi tuko pamoja. Sasa umebaki bila
Itikadi. Ile ni mali ya Mtu ni yake, nilikwambia mwache, ona sasa
unahama mara ya pili

🙆🏽‍♂️