Kilichoendelea mahakamani katika kesi ya mume anayetuhumiwa kumuua mkewe kwa kumchoma moto

Upande
wa utetezi katika kesi inayomkabili Mfanyabishara Hamisi Luongo
anayetuhumiwa kumuua Mkewe na kumchoma kwa gunia la mkaa, umeutaka
upande wa mashtaka kukamilisha uchapishaji wa jarada la kesi hiyo ya
mauaji ili shauri liendelee.


Hayo
yamebainishwa na upande wa utetezi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Salum
Ally baada ya Wakili wa Serikali, Janeth Magoho kuieleza Mahakama ya
Kisutu kuwa jarada halisi la shauri hilo lipo Polisi kwenye hatua ya
kuchapwa.

“Shauri
lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini jarada halisi lipo polisi kwenye
hatua ya uchapishaji hivyo naiomba Mahakama hii iahirishe kesi hii”-
Magoho.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi February,2020 litakapokuja kwa ajili ya kutajwa.