div class=”separator” style=”clear: both; text-align: center;”>
Mgombea ubunge kupitia tiketi ya CCM Jimbo la Longido Dkt.Stephen Kiruswa
Karibu wa CCM Wilaya ya Longido Joseph Olesadira
Mogombea ubunge kwa tiketi ya CCM akizungumza na wananchi wa kata ya Longido Mjini na ile ya orbomba katika mkutano wa hadhara uliofanyika Longido
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Longodo Joseph Olesadira akizungumza na wananchi wa Jimbo la Longido katika mkutano wa hadhara u;liofanyika jana na kushirikisha kata mbili ya Longodo
Katibu wa CCM Wilaya ya Longido Ezekilel akizungumza na wananchi wa kata ya Longido Mjini na ile ya orbomba katika mkutano wa hadhara uliofanyika Longido
Wananchi wa kata ya Longido Mjini na ile ya orbomba katika mkutano wa hadhara uliofanyika Longido wakisikiliza sera za wagombea ubunge na udiwani katika jimbo hilo
Wananchi wa kata ya Longido Mjini na ile ya orbomba katika mkutano wa hadhara uliofanyika Longido wakisikiliza sera za wagombea ubunge na udiwani katika jimbo hilo
Na.Vero Ignatus,Longido
Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Longido Dkt.Stephen Kiruswa amesema kuwa atakapochaguliwa katika Jimbo hilo kwa kushirikiana na madiwani watahakikisha wanasimamia wazawa wanapata haki ya kumiliki Ardhi, bila kuwasahau wanawake na kupata stahiki zao.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliyoandaliwa na Chama hicho kwa kata mbili za Longido mjini na Orbomba ,Kiruswa alisema kazi ya kutafuta Viongozi siyo kazi rahisi bali ni jambo gumu linalohitaji utayari kwaajili ya kuwatumia wananchi bila ubaguzi na kutatua changamoto zao ambapo yeye amesema yupo tayari .
Dkt.Kiruswa alisema kwamba kwa kushirikiana na madiwani katika Jimbo hilo mara baada ya Uchaguzi watahakikisha wanasimamia vyema maslahi ya wanalongido Ikiwemo miradi ya Afya,Maji ,Umeme,Elimu Ili kila mwananchi afaidike na miradi hiyo.
Wakizungumza wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Longido wakusema kuwa Dkt.John Pombe Magufuli amekuwa mzazi wa watoto wao kuanzia darasa la kwanza hadi sekondari kwa kuwapatia Elimu bure bila malipo na kusababisha watoto wao kung’ara kielimu
Sambamba na hayo Kamati hiyo ulisema kuwa wamekuwa wanufaika wakubwa wa maji ya mto Simba kuwafikia Longido, ikiwa ni juhudi za Magufuli na kuepuka adha ya kwenda kutafuta maji nchi jirani ya Kenya kwenye visima,kwa Sasa wanatumia maji Safi na salama.
Akizungumzia changamoto iliyokuwepo awali ya Morani kujiandikisha na kuacha kupiga kura Diwani mteule kata ya Longido Thomas Ngobei alisema kuwa tayari wameshaweka utaratibu nzuri wa zamu ya kwenda machungani kwa awamu ili wengine wapate nafasi ya kupiga kura kama haki yao ya msingi
Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Longido Ezekiel Mollel alisema kichama wana kata 18 hivyo ujio wa mgombea Urais Taifa Dkt.Magufuli Mkoani Arusha, alisema (w) hiyo wamejipanga ipasavyo kumpokea kwa kishindo
Aidha alimalizia kwa kuwataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 28/10/2020 kwaajili ya kumpigia kura Rais ,Wabunge na Madiwani wa chama cha mapinduzi kwani wananchi wenyewe wamejionea kwa macho maendeleo katika wilaya hiyo na kwa Taifa kwa ujumla.