Kuelekea uchaguzi serikali za mitaa, bukoba yakutanisha albino kujadili usalama wao

Katika kuhakikisha uchaguzi
wa serikali za mitaa unafanyika vizuri bila kuwepo kwa vitendo vya
ukatili dhidi ya watu wenye ualubino na matukio mengine yanayoweza
kuondoa amani katika jamii Ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba kwa
kushirikiana na chama cha watu wenye ualubino Bukoba (TAS) wameamua
kukutana na watendaji wa kata zote za manispaa hiyo hili kujadili namna
watakavyoweza kuwalinda hasa katika kuelekea uchaguzi wa serikali za
mitaa na uchaguzi mkuu mwaka kesho.
Akizungumza
na waandishi wa habari Afisa ustawi wa jamii manispaa ya Bukoba Japheth Musa Kanoni amesema kuwa wamefaulu kukutana tena kwenye kikao na
watendaji wa kata zote za manispaa ya Bukoba cha kujadili ulinzi na
usalama kwa watu wenye ualubino hasa kuelekea katika uchaguzi wa
serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
“Kitu
ambacho timekifanya kwa watu wenye ualibino wenyewe kwanza kuepuka
kufanya shughuli kwenye maeneo hatarishi na kitu kingine kufanya
shughuli zao mapema kwa zile ambazo ni muhimu kufanyika maana ualifu
mwingi unafanyika katika mazingira ya kificho au gizani lakini pia
wasiende mahali  kwa mda mrefu bila kutoa taarifa kwa wana familia ila
waweze kuwapatia ulinzi wao wenyewe” Alisema Japheth Kanoni.
Kwa
upande wake katibu wa chama cha watu wenye ualubino Manispaa ya Bukoba  Frolensi Felisian amesema kuwa kwa mwenendo uliopo hivi sasa hali ya usalama
imeimarika kuanzia ngazi ya wilaya mpaka kwenye mitaa na kusema kuwa
wanaimani uchaguzi utafanyika na kuisha salama.
“Niikumbushe
jamii kwa wale ambao bado wanaweza kuona alafu wakakaa kimya naomba
tuone umuhimu kama askari anavyoona mtu anafanya ualifu stand alafu
akamchukulia hatua pale pale ya kumshika na kumpeleka kituoni na katika
hili tukifanya kutoa taarifa na kushirikiana kwa pamoja tutaweza kuokoa
maisha ya watu wenye ualbino ili na wao waishi kwa amani na waweze
kujitokeza kupiga kura muda mwingine kuweza kugombea”. Alisema Frolensi
Felisian.