Rpc muroto akamata madumu ya mafuta katika basi la abiria



Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa 72 kwa makosa
tofauti likiwamo la kusafirisha mafuta ya Petrol na Diesel katika magari
ya abiria kinyume na sheria.

Akizungumza na Waandishi wa habari, ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoa
wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa polisi, Gilles Muroto, amesema, magari
matano ya kusafirisha abiria kwenda vijijini yalikamatwa yakiwa na
mafuta ya Petrol lita 1277, na Diesel lita 850, yakisafirishwa pamoja na
abiria na mizigo mingine katika Hali ya hatari.

“Katika msako uliofanyika tarehe 20/9/2019 katika kituo Cha mabasi
yaendayo vijijini eneo la kikuyu katika jiji la Dodoma yamekamatwa
mahari ya abiria matano(5) yakisafirishwa mafuta ya Petrol na Diesel na
wanaosafirisha katika njia hatarishi kwenye mahari ya abiria” amesema
Kamanda Muroto.

Pia amesema wanamshikilia Jonathan Dastani Temu mwenye (41)ambaye ni
mkazi wa Area A kwa kosa la kupatikana na Nyara za Serikali  yenye jumla
ya zaidi ya shilingi Milioni Mbili (2,875,000) aliyoipata kutokana na
uwindaji haramu.

Anasema walimkamata akiwa na nyama ya Nsya wanne na digidigi mmoja,
katika stendi mpya ya Mnadani Kizota ndani ya jiji la Dodoma.

Aidha, Kamanda Muroto ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo alihifadhi nyama
hiyo  katika mfuko wa plastiki na kuweka kwenye boxi na kusafirisha
kwenye basi ambalo linafanya safari zake kutoka  kijiji cha Makamanda
wilaya ya Manyoni mkoa wa singida kuingia Dodoma.

Hatahivyo, Kamanda Muroto  amesema wamekamatwa watu tisa (9) kwa makosa
ya unyang’anyi  wa kutumia nguvu huku zikakamatwa pikipiki 4 ambazo
zimekuwa zikitumika katika kupora watu na zilizokamatwa ni MC.660 AXD
BOXER NYEUSI,MC 154 BYG BOXER  nyeusi ,MC.569 BMZ HAOJUE nyekundu na
Watuhumiwa wanaandaliwa mashitaka na watafikishwa mahakamani.