Maalim seif sharif hamad aitwa polisi

Polisi
Mkoa wa Kaskazini Pemba visiwani Zanzibar limemtaka Mshauri mkuu wa
Chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad kufika kituo cha
Polisi Wilaya ya Wete leo Jumanne Januri 14, 2020 saa tatu asubuhi.

Mbali na Maalim Seif, mwingine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa chama hicho, Salim Bimani.

Mshsuri wa Mkuu wa Chama ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad tukiwa
tayari tunaelekea Pemba kusikiliza Wito wa Polisi huko wete Pemba.@zittokabwe @AdoShaibu pic.twitter.com/RwTfPMVJy9

— Salim Bimani (@salimbimani2) January 14, 2020