Mahakama kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi masijara ya shinyanga imeendelea kusikiliza kesi ya ugaidi

 

Na
Moshi Ndugulile

Mawakili wa upande wa
utetezi katika kesi ya ugaidi shauri namba 3 la Mwaka 2023 inayosikilizwa na Mahakama
kuu ya Tanzania masjala ya Shinyanga, wameweka pingamizi la kisheria dhidi ya
Jamhuri baada ya  maelezo ya onyo ya
mshtakiwa kuchukuliwa kinyume cha sheria,kifungu cha 58.

Mawakili wasomi wa
upande wa utetezi kwa pamoja mbele ya jaji Geofrey Isaya wameiomba mahakama
hiyo  isiyapokee maelezo ya onyo ya
mshitakiwa wa pili kama kielelezo Mahakamani hapo

Mbele ya jaji Geofrey
Isaya wakili msomi Shaaban Mvungi anayemtetea 
mshitakiwa wa pili, amesema kwa mujibu wa shahidi wa 7 wa jamhuri alimchukua
maelezo mtuhumiwa chini ya kifungu cha 58 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya
jinai namba 20,iliyofanyiwa marejeo Mwaka 2022, ambapo hata hivyo mshtakiwa hakuanzisha
yeye mchakato wa kuchukuliwa maelezo

Mvungi ameiambia mahakama
hiyo kuwa licha ya shahidi huyo kuieleza mahakama kwamba alichukua maelezo
chini ya kifungu cha 58 lakini kuna makosa mengine katika maelezo ya onyo kwa
mujibu wa sheria kifungu cha 57 kifungu kidogo cha 2 aya D,kwamba  mtuhumiwa anapochukuliwa maelezo ni lazima apewe
onyo na kuandikwa maelezo,lakini katika onyo hilo haikuonyesha muda wa kutolewa
onyo kwa mtuhumiwa

Hata hivyo Wakili Msomi
Mvungi amefafanua zaidi kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 50 maelezo hayo yalikuwa
nje ya muda

Kwa upande wake wakili
wa serikali mwandamizi Jenethreza kitaly mbele ya jaji Geofrey Isaya amesema pingamizi
la upande wa utetezi halina mashiko kwa sababu mtuhumiwa alikubali kuchukuliwa
maelezo kwa hiyari yake mwenyewe,na kwamba maelezo ya onyo yapo ndani ya muda
hivyo ameiomba maakama hiyo kuyapokea maelezo ya onyo kama kielelezo.

Akitoa ushahidi
mahakamani hapo leo septemba 14,2023 shahidi wa 7 amesema Januari 19,Mwaka 2018
mshitakiwa wa pili Hussein Juma alitoa maelezo ya onyo na kukiri kuhusika na
vitendo vya kigaidi

Shahidi huyo ameiomba
mahakama hiyo  iyapokee maelezo hayo ya
mshitakiwa wa pili kama kielelezo kwa kuwa aliyaandika chini ya kifungu cha 58
cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 ya mwaka 2002 iliyofanyiwa
marejeo mwaka 2022

Mahakama kuu ya
Tanzania Divisheni ya makosa ya rushwa na Uhujumu Uchumi masjala ya Shinyanga
imeendelea kusikiliza kesi ya ugaidi shauri namba 3 la Mwaka 2023, ambapo  Shahidi wa saba ametoa ushahidi wake.

Washitakiwa katika
shauri hilo kwa pamoja wanakabiliwana kesi ya kula njama ya kutenda vitendo vya
kigaidi kinyume na sheria ya kuzuia ugaidi namba 21 ya Mwaka 2002, ikisomwa
pamoja na aya ya 24 ya jedwali la kwanza na kifungu cha 57 kifungu kidogo cha
kwanza na kifungu cha 60 kifungu kidogo cha pili cha sheria ya uhujumu uchumi
sura ya 200 ya Mwaka 2023

Washtakiwa katika kesi
hiyo ni Salmu Haruna,Hussein Juma,Fadhir Suleiman,Rashid Mussa,Hamis
Daud,Amasha Abdallah,Nurdin Ibrahim, na Abdul Omari  wote ni wakazi wa kahama Mkoani Shinyanga,ambao
walikamatwa katika tarehe na maeneo tofauti wilayani humo

Upande wa Jamhuri
unawakilishwa na Wakili wa serikali mwandamizi Jenethreza kitaly, wakili wa
serikali mwandamizi Careny Mrango, wakili wa serikali Juma Mahona na wakili wa
serikali Shani Wampumbulya,

Mawakili wasomi wanaowatetea
washtakiwa hao ni pamoja na wakili Geofrey Tuli,wakili Shaban Mvungi,wakili
Elizabeth Luhigo,wakilim Phares Malengo,wakili Audax Costantine,wakili Getruda
Faustine,wakili Chrisantus Chengula na wakili Frank Samwel

Jaji anayesikiliza kesi
hiyo ni mheshimiwa Geofrey Isaya

Washtakiwa.Jopo la Mawakili wasomi upande wa utetezi.