Mahakama ya ictr yashindwa kubatilisha hukumu ya waziri wa rwanda

Image result for Augustin Ngirabatware


Na Queen Lema Arusha


Aliyekuwa waziri wa
mipango wa serikai ya mpito ya Rwanda  Bw. Augustine Ngirabatware
ameshindwa kuwasilisha ushahidi wa kutosha wenye uwezo wa kuaminika
katika kikao cha rufaa cha mahakama ya kimataifa inayoshughulikia
masalia ya makosa ya mauaji ya kimbari  ili kuweza kubatilisha  hukumu
ya awali anayendelea kuitumikia.

Rais wa mahakama hiyo
Jaji Theodor  Meron amesema kuwa  kupitia kifungu cha sheria namba 147
ya mwenendo wa ushuhuda Ngirabatware ambaye aliita mashahidi sita
wameshindwa kutoa ushahidi wa ukweli unaounga mkono hoja  mpya ya
kubatilisha ushahidi wa awali uliotolewa  kuwa sio wa kweli na hivyo
hukumu ya awali bado inaendelea.

Mnamo Desemba 2012
mahakama ya mauaji ya kimbari ya Rwanda (ICTR)ilimtia hatiani 
Ngirabatware kwa kosa alilolifanya mwaka 1994 la kufanya  uchochezi wa
moja kwa moja wa kufanya mauaji ya kimbari na makosa ya ubakaji na 
kuhukumiwa miaka 35 jela  na baadae Desemba 2014 mahakama ya kesi za
masalia ya makosa ya mauaji ya kimbari iliondoa kosa la ubakaji na
kubaki na kifungo cha miaka 30.

Aidha  Julai 8 mwaka
2016  Ngirabatware  aliwasilisha ombi la kupitia upya hatia yake na Juni
mwaka 2017 mahakama hiyo iliridhia  kusikiliza  kusikiliza shauri lake
upya ambapo kesi hiyo ilianza kusikilizwa september 16 hadi 27 mwaka
huu.