Makonda akabidhi milioni 40/- kwa taasisi ya moyo ya jakaya…



Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Paul Makonda na Mkurugenzi wa Puma Energy Tanzania Bw. Domonic Dhanah.
Wakicheza na watoto wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika
hospitali ya taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa
kampuni ya mafuta ya Puma Energy  Tanzania ambayo imetoa kiasi cha
shilingi milioni 40 Walipotembelea  




Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Paul Makonda akicheza na mmoja wa watoto kati ya 20 leo wanaotarajiwa
kufanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali ya taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Puma Energy
 Tanzania ambayo imetoa kiasi cha shilingi milioni 40.



Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Paul Makonda akizungumza na baadhi ya wazazi wa watoto 20 wanaotarajiwa
kufanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali ya taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Puma Energy
 Tanzania ambayo imetoa kiasi cha shilingi milioni 40.



Meneja Rasilimali Watu Kampuni ya
Puma Energy Tanzania Bi. Loveness Hoyange  akizungumza na mmoja wa
wazazi wenye watoto wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa Moyo katika
Taasisi ya Jakaya Kikwete(JKCI)kwa ufadhili wa kampuni ya Puma Energy
wenye thamani ya shilingi milioni 40.



Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Paul Makonda akicheza na mmoja wa watoto kati ya 20 leo wanaotarajiwa
kufanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali ya taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Puma Energy
 Tanzania ambayo imetoa kiasi cha shilingi milioni 40. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Puma Energy Tanzania Bw. Domonic Dhanah. Walipotembelea
 taasisi hiyo.



Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Paul Makonda akizungumza na wazazi wa baadhi ya watoto kati ya 20
wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali ya taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Puma
Energy  Tanzania ambayo imetoa kiasi cha shilingi milioni 40. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Puma Energy Tanzania Bw. Domonic Dhanah. Walipotembelea
 taasisi hiyo.



Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Paul Makonda, Mkurugenzi wa Puma Energy Tanzania Bw. Domonic Dhanah na
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)Profesa Mohamed
Janabi na wazazi wa watoto wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo
wakiwa katika picha ya pamoja.




MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda ameishukuru Kampuni ya PUMA Energy kwa kutimiza ahadi ya
kuchangia Sh. Milioni 40, kwa ajili ya kuchangia matibabu ya moyo kwa
watoto 20 wanaotibiwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini
Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya
makabidhiano ya fedha hizo leo Oktoba 3,2019 akiwa katika taasisi hiyo
Makonda amesema kazi kubwa inayofanywa na taasisi hiyo kurudisha
tabasamu kwa watoto wanaosumbuliwa na moyo haina budi kuungwa mkono na
kila mwenye uwezo.


“Wenzetu PUMA Energy wameamua kutuunga mkono, tutambue matibabu
ya moyo ni mzigo mzito kama ukisimama nao peke yako, lakini ukipata wa
kukushika mkono utauona mwepesi,” alisema.


Amesema anamshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kusimamia vema
sekta ya afya na hasa matibabu ya watoto na wagonjwa wengine
wanaosumbuliwa na moyo.


“Serikali inatoa mchango mkubwa katika kurahisisha matibabu ya
moyo ambayo ni ghali sana, awali ilikuwa lazima mgonjwa apelekwe India,
lakini sasa serikali inaokoa fedha nyingi kwa kuwafanyia upasuaji na
kuwawekea vifaa wagonjwa hapa hapa nchini,” amesema Makonda.


Wakati huo huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania
Dominic Dhanah amesema wamejionea kazi kubwa inayofanywa na JKCI katika
kuokoa maisha ya Watanzania na hasa maisha ya watoto wenye matatizo ya
moyo ambao tayari walishapoteza matumaini lakini kupitia taasisi hiyo
wamerudisha matumaini ya watoto hao kuishi.


Dhanah amesema anatambua fedha ambazo wamechangia kwa ajili ya
matibabu yasaidia kutibu watoto 20 na kuongeza wataendelea kushiriki
hatua kwa hatua kusaidia watoto wenye mahitaji na hasa ya kufanyiwa
matibabu ya moyo.


“Mnafanya kazi kubwa ya kurudisha maisha yaliyokuwa hatarini
kupotea, vilevile ninampongeza Mkuu wa Mkoa Makonda kwa kusimamia hili
kwa umakini.Tunafahamu wazazi wa watoto hawa hakuwa na fedha za
kugharamia matibabu haya lakini PUMA Energy tutaendelea kuunga mkono
hatua kwa hatua,”amesema Dhanah.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohammed
Janabi amesema kuwepo kwa taasisi hiyo kumesaidia kwa kiasi kikubwa
kuokoa fedha za Serikali kwa kuwa awali gharama za mtu mmoja kufanyiwa
upasuaji wa moyo nchini India ilikuwa dola za Marekani 15,000 ambazo ni
zaidi Sh.milioni 30.


“Kwa wagonjwa 200 tuowafanyia upasuaji ingetugharimu zaidi ya
sh.bilioni 9.4, hawa watoto mnaowaona hapa wamechangamka baada ya
kufanyiwa upasuaji, walipokuja walikuwa wanyonge kwa sababu ya maumivu
waliyokuwa nayo,” amesema Profesa Janabi na kuongeza:


“Vilevile itambulike kuwa hapa hatutibu wagonjwa wa Tanzania tu
bali wapo wengine kutoka Ethiopia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) na Malawi.”


Mmoja wa wazazi waliopeleka wagonjwa katika taasisi hiyo ambao
wamepata msaada wa Mkuu wa Mkoa Makonda, ni Joyce Cosmas kutoka mkoani
Kigoma ambaye amempeleka mtoto wake Aida Mfumya ambaye aliugua kwa muda
mrefu bila kujua kitu gani kinamsumbua.


“Nimetoka Kigoma karibu na mpaka wa Burundi, wengi wanapopimwa
na kubainika watoto wao wanasumbuliwa na moyo wanashindwa kuja Dar es
Salaamkwa sababu ya gharama kubwa, lakini kupitia Mkuu wa Mkoa Makonda
nimefanikiwa kupata matibabu,” amesema Cosmas.