Mangula:ni marufuku kwa mwanachama anayetarajia kugombea,kutoa misaada wakati uchaguzi unapokaribia

Na Amiri kilagalila-Njombe

Makamu
mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Mh.Philip Mangula amewakumbusha
wanachama wa chama hicho nchini,marufuku iliyopo kwenye katiba kwa
mwanachama yeyote anayetarajia kugombea au wakala wake kutoa misaada
mbali mbali wakati uchaguzi unapokaribia.

Philip
Mangula ametoa marufuku hiyo mkoani Njombe wakati wa kikao cha
halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kilichofanyika
katika ukumbi uliopo katika ofisi za chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe
zilizopo mjini Njombe.

Amesema
kwa mujibu wa vifungu na kanuni zilizopo kwenye katiba ya chama
zinaeleza wazi utaratibu na marufuku ya utoaji wa zawadi kwa
wanaotarajia kugombea au mawakala kutoa misaada mbali mbali wakati
uchaguzi unapokaribia kwa kuwa misaada hiyo huwa na lengo la kuvutia
kura.

“Kanuni
kifungu cha 6 kinasema ni marufuku kwa mwanachama yeyote anayetarajia
kugombea au wakala wake kutoa misaada mbali mbali wakati uchaguzi
unapokaribia,ambao ni dhahiri lengo lake ni kuvutia kura,isipokuwa
kanuni hii haijamhusu Rais,mbunge mwakilishi au diwani ambaye yuko
madarakani wakati huo kwa kuwa yeye atakuwa bado anao wajibu wa
kuhudumia eneo lake la uongozi”alisema Mangula katiba inaeleza

Awali
kabla ya kumkaribisha mwenyekiti wa CCM Tanzania bara,mwenyekiti wa
chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe Jasel Mwamwala,amewashukuru viongozi
wa chama na serikali kwa kusimamia utekelezaji mzuri wa ilani ya chama
cha mapinduzi na kuwaletea maendeleo wananchi,pamoja na kuiomba serikali
kabla ya kufika uchaguzi wa Rais kukamilisha ujenzi mkubwa wa barabara
za lami zilizoanza kujengwa mkoani humo.

“Tunaomba
hizi barabara zikamilike ili tunapofika mwezi wa kumchagua Rais bara
bara hizi zote ziwe zimekamilka na zinapitika kwasababu ndio ahadi na
wananchi wanapohoji hivi kweli hizi barabara zitakamilika?sisi tunasema
zitakamilika”alisema Jasel Mwamwala

Naye
katibu wa chama hicho mkoa wa Njombe Ndugu Paza Mwamlima amesema kwa
sasa mkoa wa Njombe unaendelea vizuri hususani kuelekea hatua za mwanzo
za uchaguzi mkuu kwa kuwa katika zoezi la maboresho na kujiandikisha
katika daftari la kudumu la mpiga kura,chama hicho kimeweza kuhamasisha
wanachama wake na kupelekea taarifa za awali kuonyesha wilaya ya Njombe
kuandikisha wapiga kura 85,508 wilaya ya Wanging’ombe wanachama 24,450
wilaya ya Ludewa 14,936 na wilaya ya Makete 14,623.

Baadhi
ya wajumbe wa kikao hicho akiwemo katibu wa siasa na uenezi mkoa wa
Njombe Erasto Ngole ametoa wito kwa wanachama wasipite kwenye kata na
majimbo ya watu kuonyesha nia ya kugombea kabla chama hakijatoa
maelekezo huku.Huku Anaupendo Gombela diwani wa kata ya Mdandu wilayani
Wanging’ombe,ametoa wito kwa wanachama kuwaacha madiwani na wabunge wao
huru kwa sasa ili watekeleze wajibu wao kabla ya mabalaza au bunge
kuvunjwa.