Mmasauni: ”utaratibu wa kuzuia mikutano ya kisiasa isiyofuata sheria uko palepale”

Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema, utaratibu wa kuzuia
Mikutano ya Kisiasa isiyofuata Sheria na taratibu upo palepale

Amesema hayo akiwa Visiwani Zanzibar alipokuwa akizungumzia hali ya
Usalama kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2019 visiwani humo

Amesema, muda wa Siasa ukifika Serikali itaruhusu mikutano hiyo yenye
lengo la kutoa nafasi kwa Wanasiasa kuzungumza na Wananchi na kueleza
kwa Wananchi walichokifanya kwa muda waliopewa baada ya kuchaguliwa na
kuteuliwa katika nafasi mbalimbali

Kuhusu hali ya usalama kwa kipindi cha 2019, amesema matukio ya mauaji
yamepungua kutoka 40 mwaka 2018 hadi 35 mwaka 2019 huku matukio ya
udhalilishaji yakiongezeka kutoka matukio 15 mwaka 2018 mpaka matukio 35
mwaka 2019.

Amesema
Serikali kupitia jeshi la polisi na mamlaka nyingine zinazohusika
limeanza harakati za kudhibiti matukio  hayo  yanayosababishwa  na 
mambo mbalimbali ikiwemo imani za kishirikina