Kasi ya maambukizo ya kirusi corona yaongezeka china

Serikali
kuu ya China imesema  kwamba idadi ya waathirika wa virusi vibaya
kabisa vya Corona imeongezeka na kufikia 2,774 kote nchini humo, huku
kukiwa na visa vipya 769 vilivyogundulika. 

Hata
hivyo ilisema hakukua na taarifa mpya za vifo iliyothibitishwa tofauti
na jimbo la Hubei, ambako mapema liliarifu watu 24 waliokufa kutokana na
maambukizi ya virusi hivyo wanafanya idadi ya waliokufa hadi sasa
kufikia 80.

 Rais
wa China Xi Jinping ameuita mripuko huo kuwa ni hali ya wasiwasi mkubwa
na kusema serikali ilikuwa inafanya juhudi za kuzuia safari na
mikusanyiko ya umma wakati ikiwapeleka wahudumu wa afya na vifaa kwenye
mji ambao ni kitovu cha janga hilo wa Wuhan.