Mawaziri wa wizara za viwanda na biashara, na wizara ya uwekezaji wakutana na kufanya mazungumzo na balozi wa marekani nchini

 

Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na wanahabari
mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani Bw.
Donald Wright ambapo wamefanya mazungumzo kuhusu fulsa za uwekezaji hapa
nchini.

Waziri
wa Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe akizungumza na wanahabari mara baada
ya kumalizika kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani Bw. Donald Wright
ambapo wamefanya mazungumzo kuhusu fulsa za uwekezaji hapa nchini.


Balozi
wa Marekani Bw. Donald Wright akizungumza wakati wa kikao na Mawawiri
wawili wa Wizara mbili Viwanda na Biashara, na Uwekezaji walipokutana
kujadili fulsa za uwekezaji hapa nchini.


Mawaziri
na Naibu Waziri wakiwa katika mazungumzo na Balozi wa Marekani Bw
Donald Wright walipokuwa wakizungumzia fursa za uwekezaji hapa nchini.


Balozi
wa Marekani Bw Donald Wright akimkabidhi kitabu Waziri wa Uwekezaji
kinachoonesha fursa mbalimbali zinazohitajika kuwekeza, mara baada ya
kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika jana April 14,2021 jijini
Dodoma,kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Prof.Kitila Mkumbo
akionyesha kitabu hicho.


Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Uwekezaji
Geoffrey Mwambe wakipitia kitabu chenye fulsa za uwekezaji
walivyokabidhiwa na Balozi wa Marekani Bw Donald Wright mara baada ya
kumalizika kwa mazungumzo.

Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo watatu kutoka kulia akiwa
katika picha ya pamoja na Waziri wa Uwekezaji Geoffrey Mwambe, na Balozi
wa Marekani Bw. Donald Wright wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya kumalizika kwa mazungumzo kuhusu fulsa za uwekezaji.

Na.Alex Sonna,Dodoma


Mawaziri
wawili wa Wizara za Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Wizara
ya Uwekezaji Geoffrey Mwambe wamekutana na kufanya mazungumzo na Balozi
wa Marekani hapa nchini Bw. Donald Wright kwa lengo la kujenga
ushirikiano na kushirikishana fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa
nchini.


Akizungumza
na waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo hayo Waziri ya Viwanda
na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amesema katika mazungumzo yao wamelenga
kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi mbili za Tanzania na
Marekani.


“Leo
tumekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw.
Donald Wright, kuona namna ya kukuza ushirikiano wetu uliopo baina ya
nchi hizi mbili, bado tunafursa nyingi na kubwa za wafanyabiashara wetu
kutumia fursa hiyo” amesema Prof. Mkumbo.


Amesema
katika mazungumzo hayo wamekubaliana kuweka jitihada za kuhakikisha
nchi hizo mbili zinazidi kushirikiana katika nyanja za kiuwekezaji na
kuleta manufaa na kuwawezesha wafanyabiashara kuwanya biashara kukuza
uchumi wa nchi na mtu mmoja moja.


Amesema
katika mazungumzo hayo pia wamezungumzia kuhusu mazao ya kimkakati hasa
katika kuchakata na sio kuuza malighafi, na hatimaye mazao hayo
yachakatwe hapa nchini na kuuza bidhaa badala ya kuuza malighafi, na
sekta ya matunda ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.


Nae
Waziri wa Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe amesema katika mazungumzo hayo
pia wamezungumza kuhusu uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwamo ya
afya hapa nchini, na wameonekana kuridhika na hatua mbalimbali
zilizochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika uwekezaji.


Amesema
wawekezaji kutoka Marekani wameonyesha wapo tayari kuja kuwekeza hapa
nchini ambapo tayari kuna kampuni imeonyesha nia ya kuja kuwekeza katika
sekta ya mawasiliano kwa kuwekeza katika kampuni ya simu, na kampuni ya
utalii kutoka Arusha imeonyesha nia ya kutaka kuongeza zaidi uwekezaji.


Ameongeza
kuwa “Tumeongelea uchakataji wa mazao na ukiangalia Marekani ananunua
korosho nchi flani, na ukiangalia sisi tunauza korosho ghafi na hizo
nchi zinachakata na kuuza marekani, na sisi sasa tunaweza kuzichakata
hapa nchini na kuuza Marekani” amesema Waziri Mwambe.


Amesema
pia yapo mazao mengine ya kumkakati kama Kahawa na Pamba ambayo
yatachakatwa na kuuzwa nje ya nchi hatimaye kama nchi kupata mapato
kupitia kodi na kukuza ajira kwa wananchi ambao watapata ajira katika
viwanda hivyo vitakavyoanzishwa.


Amesema
katika mazungumzo hayo wamekubaliana kufanya majadiliano mara kwa mara
ili kuuisha makubaliano yao ambapo watakuwa wakifanya tathmini kuona
makubaliano hayo yanavyofanya kazi katika kuimarisha ushirikiano uliopo
kwa miaka sitini sasa baina ya haya mataifa mawili.


Kwa
upande wake Balozi wa marekani nchini Tanzania Mhe. Donald J. Wright
amefurahishwa na ushirikiano wa kudumu wa Zaidi ya miaka 70 uliopo kati
ya Tanzania na Marekani na


Mhe.Wright
ameahidi kuwa Serikali ya Marekani itashirikiana kwa dhati na kwa
karibu na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wawekezaji
kutoka marekani wanakuja kuwekeza nchini Tanzania kwani nchi hii ina
fursa nyingi za uwekezaji pamoja na hali nzuri ya ulinzi na usalama.
Balozi Mhe. Wright amesema kuwa Marekani imetengeneza historia kubwa
katika kusaidia maendeleo ya Tanzania katika miradi ya kupambana na
magonjwa, Ulinzi, elimu, miundombinu n.k ambapo hiyo imepelekea uhusiano
kati ya Marekani na Tanzania kuimarika zaidi.