Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul
(kushoto) akizungumza leo katika kikao cha Mawaziri wa Wizara ya
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na Wizara hiyo cha kujadili
hoja zinazohusu utekelezaji wa majukumu ya Sekta hizo ya kisera,
kisheria na kikanuni kwenye masuala ya mawasiliano nchini kilichofanyika
jijini Dodoma, anayefuata ni Waziri wake Innocent Bashungwa akifuatiwa
na Waziri waMawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile
na kuliani Naibu wake Mhandisi Kundo Mathew.
Kikao hicho
kimefanyika kufuatia maelekezo yaliyotolewa hivi karibuni na Mheshimiwa
SamiaSuluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yakutaka
kufanyika marekebisho ya Sheria na Kanuni zinazosimamia Vyombovya Habari
hapa nchini hususan Televishen Mtandao (Online TV)
Wajumbe wa kikao cha Mawaziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari pamoja naWizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Dkt. Hassan Abbas akizungumza katika kikao hicho cha kujadili
hoja zinazohusu utekelezaji wa majukumu yaSekta hizo ya kisera, kisheria
na kikanuni kwenye masuala ya mawasiliano nchini kilichofanyika jijini
Dodoma leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.
Hassan Abbas (kushoto), akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula akifuatiwa na
Naibu wake Dkt. Jim Yonaz katika kikao cha Mawaziri wa Wizara hizo mbili
cha kujadili hoja zinazohusu utekelezaji wa majukumu ya Sekta hizo ya
kisera, kisheria na kikanuni kwenye masuala ya mawasiliano nchin
ikilichofanyika jijini Dodoma leo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas
(kushoto) akizungumza leo katika kikao cha Mawaziri wa Wizara hiyo na
Wizara ya Mawasiliano naTeknolojiaya Habari cha kujadili hoja zinazohusu
utekelezaji wa majukumu ya Sekta hizo yakisera, kisheria na kikanuni
kwenye masuala ya mawasiliano nchini kilichofanyika jijini Dodoma.Kulia
ni Katibu Mkuu waWizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.
Zainab Chaula. Kikao hicho kimefanyika kufuatia maelekezo yaliyotolewa
hivi karibuni na Mheshimiwa SamiaSuluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania yakutaka kufanyika marekebisho ya Sheria na Kanuni
zinazosimamia Vyombo vya Habari hapa nchini hususani Televishen
Mtandao (Online TV)
Na John Mapepele, Dodoma
Waziri
anayesimamia Sekta ya Habari Mhe. Innocent Bashungwa na Waziri anayesimamia
Sekta ya Mawasiliano Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na timu ya Makatibu Wakuu na Wataalam wa Wizara hizo wamekaa na kujadili hoja mbalimbali kuhusu utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za
kisekta kufuatia maelekezo ya hivi karibuni ya Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maelekezo hayo aliyatoa
wakati wa kuwaapisha Makatibu
Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na
Wakuu wa Taasisi ya kufanya marekebisho ya Sheria na Kanuni zinazosimamia Vyombo vya Habari hususan
Televisheni Mtandao (Online TV).
Majadiliano
hayo yamefanyika jijini Dodoma Aprili 14, 2021 na kutoa mapendekezo ya hatua za
kuchukuliwa kwenye hoja 13 zilizoainishwa na Wizara hizo.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa amesema miongoni mwa maazimio
yaliyofikiwa ni pamoja na kufanya mapitio ya Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo
katika maeneo yote yenye mapungufu ili
ziendane na hali halisi ya sasa na
kuweka mifumo rafiki ya
kushughulikia masuala yote yanayohusu sekta ya Mawasiliano na Utangazaji
“Tumeagiza
Wataalam wafanye uchambuzi wa Kanuni za Maudhui Mtandaoni ili kuona kama zinaendana
na mazingira ya sasa” amesisitiza Waziri Bashungwa
Ameongeza kuwa Wizara
zimeaazimia kuja na mkakati wa kuwaelimisha
wadau wa Sekta hizo ili kudhibiti makosa
ya kimaudhui yanayofanywa na Vyombo vya Habari badala ya hali ilivyo
sasa inayotoa adhabu kali zinazojikita kwenye utozaji wa faini kubwa pamoja na
kufungiwa.
Suala lingine ambalo
limeazimiwa kufanyiwa kazi ni chaneli za bure kutoonekana kwenye visimbusi
ambavyo kimsingi zinapaswa kuonekana hata pale kifurushi kinapokuwa kimeisha
muda wake.
Kwa upande wake Waziri wa
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile
amesema kukua kwa teknolojia kumewezesha kukua kwa matumizi ya huduma za
mawasiliano yakiwemo ya utangazaji hivyo katika kipindi kifupi kijacho Serikali kupitia
Wizara hizo mbili itafanya maboresho
makubwa kwenye kanuni husika ili
kuendana na hali halisi ya sasa.
Ameongeza kuwa Serikali ilitunga Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo
mbalimbali zikiwemo Sheria ya huduma za Habari Namba 12 ya mwaka 2016, Sera ya
Habari na Utangazaji ya mwaka 2003 na Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016
ambazo pamoja na mambo mengine zinaelekeza kuweka mazingira wezeshi ya kukuza
maudhui ya ndani (Local content).