Kiongozi wa mbio za bendera Wilaya ya Shinyanga, katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Bwana Ally Bin Ally (Majeshi) akiwa ameambatana na viongozi wengine amekimbiza na kusimika Bendera za CCM kwa mabalozi katika kata ya Kambarage Jimbo la Shinyanga mjini.
Imesimikwa Bendera ya CCM kwa balozi wa Mwasele Mihogoni Bwana Majiya Mwandu, imesimikwa Bendera ya CCM kwa balozi Edis Maridadi wa mtaa na tawi la Mwasele B, imesimikwa Bendera ya CCM kwa balozi Mgeni Ally pamoja na tawi la Kambarage.
Kiongozi wa mbio za Bendera Wilaya ya Shinyanga Ally Bin Ally (Majeshi) baada ya kusimika Bendera hizo amewataka mabalozi kuzisimamia na kuzilinda Bendera hizo ili ziweze kudumu Miaka mingi huku akiwasisitiza kutoziondoa kwenye maeneo yao.
Wakati mbio za Bendera zikiendelea kiongozi wa mbio hizo ambaye ni mkatibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga B wana Ally Bin Ally (Majeshi) pamoja na viongozi wengine wamekagua uhai wa wanachama huku wakitoa maagizo viongozi wa mashina kuendelea kuongeza wanachama wapya.
Wamekagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo wamewapongeza viongozi kwa kuimarisha umoja wao pamoja na ushirikiano baina yao na wananchi katika kata hiyo ya Kambarage.
Baada ya mbio za Bendera katika kata hiyo pia kimefanyika kikao cha ndani kilichojumuisha viongozi wa chama cha mapinduzi ngazi za matawi na kata pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa na Diwani wa kata ya Kambarage Mhe. Hassan Mwendapole ambapo viongozi ngazi ya Wilaya wametoa maelekezo mbalimbali na kusisitiza yazingatiwe ili kuepusha migogoro na kero kwa wananchi.
Aidha baada ya kikao cha ndani umefanyika mkutano wa hadhara uliojumuisha wananchi wa kata ya Kambarage ambapo pamoja na mambo mengine viongozi wameeleza mambo mazuri yaliyofanywa na viongozi ngazi ya juu huku wakimpongeza Rais Dkt. samia Suluhu Haasan, mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Paschal Patrobas Katambi pamoja na Diwani wa kata ya Kambarage Mhe. Hassan Mwendapole kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM.
Katibu wa umoja wa vijana UVCCM Wilaya ya Shinyanga Bwana Naibu Katalambullah katika ziara hiyo pamoja na mambo mengine amesisitiza viongozi kupendana, kushirikiana na wananchi huku akiwaomba wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na viongozi wa chama na serikali katika kutela maendelea.
Amesema kila mmoja anawajibu wa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na viongozi wa serikali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa lengo la kutatua changamoto na kuinua uchumi wa wananchi.
Katibu wa jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Doris Yotham Kibabi ametumia nafasi hiyo kuwataka wazazi na walezi kuwalea watoto wao katika misingi na maadili mema ikiwemo kuwapa haki yao ya elimu kwa kuhakikisha wanawasomesha ili kuendelea kuwa na Taifa bora lenye vijana wasomi.
Kwa upande katibu wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Sharifa Hassan Mdee amekemea tabia za watu kuwafanyia ukatili watoto huku akiitaka jamii kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo vya ukatili ili hatua za kisheria ziwezi kuchukuliwa na mamlaka husika.
Diwani wa kata ya Kambarage Mhe. Hassan Mwendapole amesema changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ataendelea kuzitatua ikiwemo kuwasilisha changamoto hizo kwenye baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili ziweze kuingizwa kwenye bajeti ikiwemo miundombinu ya barabara.
Diwani Mhe. Hassan Mwendapole pamoja na mambo mengine amewaomba wananchi wa kata ya Kambarage kuendelea kuchukua tahadhara ya mvua kubwa zilizotajwa na mamlaka ya hali ya hewa Tanzania, ambapo amesema ni muhimu wananchi kuwa na tahadhari ikiwemo kutunza miundombinu ya barabara ili mitaro iweze kupitisha maji.
Naye katibu wa CCM kata ya Kambarage Bwana Hamis Kabuta ameahidi kuyasimamia maelekezo yote yaliyotolewa na viongozi wa CCM Wilaya ya Shinyanga ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na chama cha mapinduzi hasa katika kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa Mwaka 2024 pamoja na uchaguzi mkuu 2025.Mbio za bendera ya CCM zikiendelea katika maeneo mbalimbali ya kata ya Kata ya Kambarage Jimbo la Shinyanga mjini ambapo kiongozi wa mbio za bendera Wilaya ya Shinyanga ni katibu wa CCM Wilaya hiyo Bwana Ally Bin Ally (Majeshi).