Mbunge mzava awataka watanzania kuendelea kuienzi na kuitunza amani

MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Thimotheo Mzava kushoto
akimkabidhi Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa ambaye
ni Diwani wa Kata ya Majengo(CCM) Mustapha Shengwatu tuzo ya kutambua
mchango mkuu huyo wa wilaya katika jamii ya wilaya hiyo juzi
uliotunukiwa na Taasisi ya Korogwe Commnunity Foundation wakati wa
uzinduzi wake kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo  Magesa Kuboja Sijo

MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Thimotheo Mzava kushoto
akimkabidhi Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa ambaye
ni Diwani wa Kata ya Majengo(CCM) Mustapha Shengwatu tuzo ya kutambua
mchango mkuu huyo wa wilaya katika jamii ya wilaya hiyo juzi
uliotunukiwa na Taasisi ya Korogwe Commnunity Foundation  wakati wa
uzinduzi wake kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo  Magesa Kuboja Sijo

 MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Thimotheo Mzava akizungumza wakati wa uzinduzi huo

 Mkurugenzi wa Taasisi ya  Korogwe Commnunity Foundation Magesa Kuboja Sijo akizungumza wakati wa uzinduzi huo


 Diwani wa Kata ya Majengo(CCM) Mustapha Shengwatu akizungumza wakati wa uzinduzi huo

MBUNGE
wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Thimotheo Mzava kushoto akimkabidhi
cheti cha kutambua mchango wa Taasisi ya Korogwe Community Foundation
mmoja wa vijana kushoto ni Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Korogwe

SEHEMU ya waalikwa kwenye uzinduzi wa Taasisi hiyo

MBUNGE
wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Thimotheo Mzava katika akiwa kwenye
picha ya pamoja na baadhi ya vikundi vya Kwaya mara baada ya kuzindua
Taasisi hiyo

Kwaya ya Maranatha ya wilayani Korogwe Mkoani Tanga ikitumbuiza wakati
wa uzinduzi wa Taaisis ya Korogwe Community Foundation uliofanyika mjini
humo
MBUNGE wa
Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Timotheo Mzava amewataka watanzania kuendelela
kuienzi na kuitunza amani iliyopo hapa nchini kwani ni tunu kubwa .

Mzava
aliyasema hayo juzi mjini Korogwe wakati akizundua Taasisi ya Korogwe Community
Foundation ambapo alisema kwamba lazima watanzania wasimame imara kwa maombi
ili kumuomba mwenyezi Mungu aendelee kuifanya nchi kuwa na utulivu uliopo hivi
sasa.

Mbunge
huyo aliipongeza Taasisi hiyo ya Korogwe Community Foundation kwa mawazo
waliyokuwa nayo ambayo yamezaa kitu kikubwa ambacho kimekuwakutananisha na ndio
mambo anayoyatamani kuyaona huku akihaidi kuwaunga mkono kwenye dhamira yao
hivyo.

Alisema
kwani nchi ikikosa amani nchi hakuna watakaosoma, watakaofanya kazi,
watakaozalisha na hivyo kupelekea uchumi kudodora hivyo tuendelea kumuomba mungu
aendelee kuitunza na kulitabariki Taifa letu ili kuendelkea kubarikiwa kwenye
shughuli zinazofanyika.

“Lakini
pia tuendelee kuwaombe viongozi wetu akiwemo Rais na viongozi wengine kuwaombea
waendelea kuwa na afya njema na kutimiza majukumu yao kwani wanafanya kazi
kubwa sana kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi”Alisema Mbunge Mzava.

“Pia nyie
waimbaji pamoja na kuimba kwenye makanisa na shughuli natamani vikundi vya
kwaya viwe na Tassisi ambazo zinaweza kuwasaidia jamii na kuwa sehemu ya
kujisaidia nyie wenyewe na jamii zenu”Alisema

Uzinduzi
huo ulikwenda sambamba na tukio la utoaji tuzo kwa kutambua mchango wa viongozi
wa dini na serikali kutokana na kwamba kama kusingekuwepo na dini nchi
isingekuwa na utulivu kama ilivyokuwa leo.

“Mnatusaidia
sana sana kwenye kuponya na kulea roho zetu…kutusaidia kuwashika na
kutusaidia waumini wetu tunatambua mchango wenu na mnafanya kazi kubwa na nzuri
tunaitambua kama mnavyoshirikiana na taasisi ya Korogwe Community iendelee
kushirikiana na viongozi wa serikali”Alisema Mbunge huyo.

Awali
akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Taasisi ya Korogwe Community
Foundation Magesa Kuboja Sijo alisema kwamba taasisi hiyo imekuwa ikifanya
mambo mbalimbali ya kijamii wilayani humo ikiwemo kuwasaidia wananchi
wanaokumbana na changamoto mbalimbali.

“Lakini
kwenye tukio la leo tumekutana hapa kwa madhumbuni makubwa ya kufunga mwaka na
uzinduzi wa Taasisi ya Korogwe Community Foundation tulianza kama kikundi na
sasa tutafanya kazi Tanzania nzima na tumekusanyika kupongezana na kushikana
mikono “Alisema

Hata
hivyo alisema pia lengo la pili la kukutana ni kufahamiana watumishi wa mungu
hasa waimbaji kwenye Tamasha ikiwemo kuwapongeza watumishi wa mungu wachungaji,
maaskofu, mapadre ambao wanafanya kazi kubwa ya kuliombe taifa wakati watu
wamelala majumbani.

Naye kwa
upande wake akizungumza wakati wa uzinduzi huo Askofu wa Kanisa la Evangelisti
Assemblies Of God Majengo wilayani Korogwe Samweli Shemzigwa aliitakia
mafanikio mema Taasisi huyo huku akiwatakia heri mwenyezi mungu andelee kuwainua
kiuchumi kwa kuweza kupata kibali.