Mhe.ikupa atekeleza ahadi yake kwa kuwasaidia watu wenye ulemavu vifaa saidizi

 

 



 

Mbunge
wa Viti Maalum UWT (watu wenye ulemavu) Mhe.Stella Ikupa ametekeleza
ahadi yake ya kukabidhi vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu ambapo
ametoa jumla ya Baiskeli za watu wenye ulemavu 10 zenye thamani ya hela
za Kitanzania milioni nne(4,000,000).


Mhe.Ikupa
amekabidhi Baiskeli kwa kijana Marcos Venas aishie kata ya Kimara
ambaye aliahidi kumsaidia kijana huyo hivyo ametekeleza ahadi yake
kwake huku Mama wa Kijana huyo ametoa shukrani kwa Mhe.Ikupa na Uongozi mzima
wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mhe.Rais Dkt.Magufuli kwa kuonesha
kweli ni wenye kutekeleza ahadi zao kwa haraka katika kuwajali wananchi
wote.

Pia
Mhe.Ikupa amekabidhi Baiskeli 3 kwa kituo cha kulea watoto wenye
ulemavu kiitwacho SALT kilichopo kata ya Mbezi ambapo awali alitoa ahadi
ya kumsaidia mtoto mmoja aliyekuwa na uhitaji wa baiskeli hiyo siku ya
tarehe 13 mwezi Disemba mwaka jana katika Bonanza la michezo la
lililokuwa limelenga kusaidia katika uwezeshaji wa kupata vifaa saidizi
ambapo amekamilisha ahadi hiyo na kuongeza baiskeli 2 za ziada kwa kituo
hicho.

Mkurugenzi wa kituo hicho Bi.Rebeca Leby ametoa shukrani kwa
Mhe.Ikupa kwa juhudi zake katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wenye
uhitaji wa vifaa saidizi wanapata ama kuwezeshwa katika kupata vifaa
hivyo.


Aidha
Mhe.Ikupa amekabidhi baiskeli moja kwa mtoto Salome Asumwike wa Darasa
la pili katika shule ya msingi Kalakata ambaye analelewa na Bw.Axon na
Bi.Sophia ambao wamemshukuru Mhe.Ikupa kwa kukamilisha ahadi yake ya
kumsaidia kijana huyo katika kumpatia baiskeli hiyo ya kumuwezesha
kusogea sehemu moja hadi nyingine.

 

Mhe.Ikupa
aliahidi kushirikiana na waheshimiwa madiwani akiwemo diwani wa viti
maalum Mhe.Magreth Cheka kuwezesha kujenga choo kitakachokuwa rafiki na
wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya Karakata. Tatizo hili lilielezwa
kwa mbunge Ikupa kuwa mtoto Salome anapata shida sana akiwa shuleni
kwani hakuna kabisa choo rafiki katika shule ya Karakata


Pia
Mhe.Ikupa ametekeleza ahadi yake kwa kumkabidhi baiskeli saidizi kijana
Andrew Sajusi mkazi wa Yombo vituka ambapo amefuatana na Mhe.Mariam
Mbunge wa Viti maalum ambaye ndiye aliyemtambulisha kijana Sajusi kwa
mhe.Ikupa

Pia Mhe.Ikupa amempatia mtoto Iddy Halid baiskeli saidizi mkazi wa
kata ya Tabata ambapo Mama mlezi wa mtoto huyo Bi.Zainabu amemshukuru
Mhe.Ikupa kwa kutimiza ahadi hiyo lakini kwa kuonesha utu na upendo wa
hali ya juu pamoja na kujituma kwake katika kusaidia watu wenye ulemavu.

 

Zoezi hili liliendelea katika kata ya Majohe, Mhe.Ikupa alikutana na
watu wenye ulemavu na wazazi wa watoto wenye ulemavu wapatao 140 akiwa
amefuatana na waheshimiwa madiwani wa viti maalum watokao Jimbo la
Ukonga ambapo ametoa baiskel 2, pampasi na nepi kwa watoto wenye
ulemavu.Mhe.Ikupa ameahidi kuongeza baiskel zingine tano katika kata hii
ya Majohe na 1 katika kata ya Tabata.

Mhe.Ikupa alitoa ufanunuzi kuwa zoezi hili ni endelevu kwa nchi
nzima” zoezi hili litakuwa endelevu kwa nchi nzima, ninategemea panapo
uzima nitaendelea kutoa baiskel, bajaji, pikipiki, mafuta ya ngozi kwa
watu wenye ualbino n.k”.

Katika mkutano huu alipokea changamoto
mbalimbali za watu wenye ulemavu, ikiwemo uhitaji wa miguu bandia ambapo
aliwaelekeza wajiandikishe wahitaji na yeye atawapeleka kwa wadau
wanaotoa miguu hiyo.

 Pia aliweza kuahidi kumnunulia brenda mama mwenye mtoto mwenye ulemavu ambaye hawezi kula vyakula vigumu


Katika zoezi hili baiskel 1 ilitolewa kwa mtoto mwenye ulemavu Mkoani Morogoro.


Katika zoezi hili la utekelezaji wa ahadi,Mhe.Ikupa pia ameongozana na uongozi wa UWT kata zote katika maeneo yote aliyofika

Mbunge
wa Viti Maalum UWT (watu wenye ulemavu) Mhe.Stella Ikupa akizungumza wakati wa halfa hiyo