Mhe. katambi azindua rasmi malula tv

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi
ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi,
mgeni rasmi katikati akizindua rasmi taasisi ya habari za mtandaoni Malula TV
usiku wa kuamkia leo siku ya Jumanne Julai 11,2023.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi
ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi
amempongeza Daniesa Malula kwa kuanzisha Online TV taasisi ambayo itatoa ajira
kwa vijana Nchini.

Mhe. Katambi ameyasema hayo akiwa mgeni rasmi kwenye
hafla ya uzinduzi rasmi wa Malula TV iliyofanyika katika ukumbi wa Malula
Center uliopo kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Hafla hiyo imefanyika usiku wa kuamkia leo Jumanne
Julai 11,2023 na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, taasisi binafsi pamoja,
wadau mbalimbali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.

Mbunge Mhe. Katambi pamoja na mambo mengine ametumia
nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa Malula TV kwa ubunifu na uthubutu wake wa
kuambua kuanzisha taasisi ya habari ambayo itatoa fursa mbalimbali hasa kwa
vijana Nchini.

Katambi amemsihi Mkurugenzi wa Malula TV, Bwana
Daniesa Malula kutokukata tamaa huku akimsisitiza kutekeleza majukumu yake kwa
kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za Nchini.

Aidha Mhe. Katambi ameahidi kuendelea kushirikiana
naye ambapo amesema atahakikisha changamoto zilizopo anazipunguza au kumaliza
kabisa ndani ya muda mfupi ili kutekeleza majukumu yake bila vikwazo.

Ametumia nafasi hiyo pia kuwaomba vijana wengine
Nchini kuiga mfano huo wa Bwana Daniesa Malula kwa lengo la kuinua uchumi wao
na Taifa kwa ujumla.

Baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali ikiwemo Naibu
meya wa Manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ndala Mhe. Zamda
Shabani pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Jonathan
Madete wamempongeza Mkurugenzi wa Malula TV, Bwana Daniesa Malula kwa
kufanikiwa kuanzisha taasisi ya habari ambayo itasabaza habari mitandaoni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Malula TV, Bwana Daniesa
Malula amesema taasisi yake atahakikisha inatekeleza majukumu yake kwa
kuzingatia sheria na kanuni za tasnia ya habari Nchini.

TAZAMA PICHA ZOTE

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi
ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi
awali akipokelewa na Mkurugenzi wa Malula Tv Bwana Daniesa Malula upande wa
kulia.