Miili ya askari waliofariki kwa ajali njombe yaagwa na mamia ya wananchi

Na Amiri kilagalila-Njombe
Mamia ya wananchi wamejitokeza hii leo katika viwanja vya jeshi la
polisi mkoani Njombe kuaga miili ya askari watatu waliofariki katika
ajali mapema alfajiri ya tarehe tatu ambapo ajali hiyo imehusisha basi
la abiria kampuni ya sharon lenye namba za usajiri T349 CXD na gari la
polisi lenye namba za usajili pt 3734.


Askari
waliofariki katika ajali hiyo ni namba H 4401 Marianus Said
Hamissi,namba H6802 pc Michael Mwandu na askari namba H 7486 pc Hery
Athmani ambapo wote wamesafirishwa kuelekea makwao kwaajili ya mazishi

Akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari hao mkuu wa mkoa wa Njombe
Cristopher Ole Sendeka amesema, serikali imepoteza vijana mhimu ambao
wamefariki wakati wakienda kulitumikia taifa na kuwataka askari wengi
kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

“Ajali hii imeondoa vijana wetu watatu,wawili wapo Moi tumewakimbiza
jana kwa ndege na wengine wapo kwenye hospitali yetu ya kibena na hakika
vyombo vyote vitasimamia kujua ukweli wa tukio hili na aliyefanya
dhambi hii kwa uzembe atachukuliwa hatua za kisheria”alisema Ole Sendeka

Hamis  Issa ni kamanda wa polisi mkoa wa Njombe amewashukuru wakazi wa
mkoa wa Njombe kwa kujitokeza kwa wingi pamoja na kujitolea michango yao
kuhakikisha askari wote waliofariki wanasafirishwa kuelekea kwao
kwaajiri ya mazishi.

“Wananchi mmeonyesha ni jinsi gani mna upendo na vijana wenu,na hawa
waliofariki kwa kweli wamefariki wakiwa wanaenda kutimiza jukumu la
kisheria,tunawashukuru sana”alisema Hamis Issa

Solanus Mhagama ni mmoja wa wakazi mkoani hapa ameonyesha kusikitishwa
na kifo cha askari hao ambao walikuwa bado vijana wadogo na hivyo
kuiomba serikali kuweka matuta pamoja na kutanua barabara hiyo ili
kuepusha ajali katika eneo hilo ambalo lina mlima mkali.

Ajali hiyo iliyosababaishwa na mwendokasi wa gari ya abiria ilipelekea 
vifo  vitatu vya askari wa polisi kikosi cha kutuliza gasia mkoani
Njombe huku wengine tisa wakiendelea na matibabu katika hospitali ya mji
Njombe Kibena na hospitali ya taifa Mhimbili.

Ibada ya kuagwa miili hiyo imehudhuliwa na viongozi wa dini mbalimbali
ambapo wametumia fulsa hiyo kuwa taka wananchi kufuata sheria za usalama
barabarani ili kuepuka ajali zinazosababishwa  na uzembe.