Na. Peter Haule na Josephine Majula, WFM, Dodoma
Serikali
imeuomba Umoja wa Ulaya (EU) kuwekeza katika maeneo ya maendeleo ambayo
tayari Serikali imeanza kuyatekeleza ikiwemo uboreshaji wa miundombinu
katika mkataba mpya wa ushirikiano kati ya Tanzania na EU kwa mwaka 2021
hadi 2027.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya
(EU) nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti, kuhusu ushirikiano wa
maendeleo ya kiuchumi.

Dkt. Mpango alisema kuwa, katika mkataba mpya wa ushirikiano wa kiuchumi
kati ya Tanzania na EU unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka 2021 ni
vema ukaendelea kuimarisha maeneo ya maendeleo ambayo tayari yameanza
kutekelezwa na Serikali hususani katika Sekta ya Elimu, Afya,
miundombinu na mingine ili kufikia malengo endelevu.

“Tuna kazi kubwa ya kuwekeza kwenye rasilimali watu kwa kuwa miradi kama
miundombinu haiwezi kufikia malengo yake bila kuwa na uwekezaji katika
rasilimali hiyo na ndio maana kama Serikali tumeamua kutoa elimu bure
kuanzia shule ya Msingi hadi Sekondari”, alieleza Dkt. Mpango.

Alisema kuwa katika suala la miundombinu, Serikali inaangalia uwezekano
wa kuanza ujenzi wa Reli kutoka Bandari ya Mtwara katika Bahari ya Hindi
hadi Bandari ya Mbamba Bay katika Ziwa Nyasa, ili kurahisisha
usafirishaji wa bidhaa na kuokoa fedha nyingi zinazotumika kukarabati
barabara zinazoharibika kwa usafirishaji wa bidhaa kwa njia ya barabara.

Aidha alieleza kuwa miundombinu hiyo ya reli itakuwa na matawi kuelekea
Liganga ambako kunapatikana madini ya Chuma na Mchuchuma ambako kuna
hazina kubwa ya Makaa ya Mawe.

Alisema Reli hiyo itasaidia pia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa
kwenda nchi jirani ikiwemo Malawi, hivyo kuchochoa biashara na kuongeza
mapato.

Kwa upande wake Balozi wa EU nchini Tanzania, Mhe. Manfredo Fanti,
aliipongeza Serikali kwa kuwa na Sera nzuri za maendeleo lakini pia
akasema kuwa ili kuboresha mazingira ya kibiashara, miongoni mwa mambo
yanayohitajika ni pamoja na Miundombinu, mafunzo, kuwa na uchumi wa
kidigitali na siasa bora, mambo ambayo Tanzania imepiga hatua kubwa
katika kuyatekeleza.

Mkataba wa ushirikiano wa maendeleo ya kiuchumi uliokuwa ukitekelezwa
kuanzia mwaka 2014 unamalizika mwaka huu ilihali kwa sasa kunatarajiwa
kuwepo kwa majadiliano ya mkataba mwingine wa ushirikiano unatarajia
kuanza kutekelezwa mwaka 2021 na kumalizika 2027.

Katika tukio jingine, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
namekutana na mkufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikianao wa Biashara
wa Finland, Mhe. Ville Skinnari, ambapo walijadili mambo mbalimbali
yakiwemo masuala ya ushirikiano na maendeleo ya kiuchumi.