Mkoa wa shinyanga waadhimisha siku ya mashujaa

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwenye maadhimishi ya siku ya mashujaa.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkoa wa Shinyanga umeungana na Mikoa
mingine Nchini kuadhimisha siku ya Mashujaa kitaifa ambapo  serikali imesema kwa kutambua na
kuthamini  mchango wao, itaendelea  kuwakumbuka na kuwaenzi Mashujaa wote wa
Tanzania walipoteza maisha wakati wakipigania 
Taifa lao

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga, kwenye maadhimisho ya siku ya mashujaa yaliyofanyika Mjini
Shinyanga, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amesema ni wajibu wa
kila mtanzania kuwakumbuka mashujaa wote ambao walijitoa mhanga kupambana dhidi
ya ukoloni kwa ajili ya maslahi ya Taifa

Amesema kwa kutambua mchango mkubwa
wa mashujaa hao serikali iliweka siku maalumu ya kuwakumbuka mashujaa hao kama
ishara ya kuwaenzi

Afisa Mteule Daraja la Pili Thomas
Nyabitwano ni Askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambaye ni mmoja
wa mashujaa waliopigana vita vya kagera dhidi ya Uganda mnamo Mwaka 1978.

Amewaomba askari wa Jeshi la
wananchi wa Tanzania kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu
huku wakitanguliza mbele uzalendo  kwa
maslahi mapana ya Taifa la Tanzania

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Watemi
Mkoa wa Shinyanga Chief Kidola Njange ameomba watanzania hasa vijana kuendelea
kuilinda na kuidumisha amani ya Tanzania.

Julai 25, ya kila Mwaka watanzania
huadhimisha kumbukumbu ya siku ya Mashujaa wa Tanzania.

Maadhimisho ya siku ya Mashujaa
yakiendelea katika mnara wa mashujaa 
Mkoani Shinyanga leo Jumanne Julai 25,2023.

Maadhimisho ya siku ya Mashujaa
yakiendelea katika mnara wa mashujaa 
Mkoani Shinyanga leo Jumanne Julai 25,2023.

Maadhimisho ya siku ya Mashujaa
yakiendelea katika mnara wa mashujaa 
Mkoani Shinyanga leo Jumanne Julai 25,2023.

Maadhimisho ya siku ya Mashujaa
yakiendelea katika mnara wa mashujaa 
Mkoani Shinyanga leo Jumanne Julai 25,2023.

Maadhimisho ya siku ya Mashujaa
yakiendelea katika mnara wa mashujaa 
Mkoani Shinyanga leo Jumanne Julai 25,2023.

Maadhimisho ya siku ya Mashujaa
yakiendelea katika mnara wa mashujaa 
Mkoani Shinyanga leo Jumanne Julai 25,2023.

Maadhimisho ya siku ya Mashujaa
yakiendelea katika mnara wa mashujaa 
Mkoani Shinyanga leo Jumanne Julai 25,2023.

Maadhimisho ya siku ya Mashujaa
yakiendelea katika mnara wa mashujaa 
Mkoani Shinyanga leo Jumanne Julai 25,2023.

Maadhimisho ya siku ya Mashujaa
yakiendelea katika mnara wa mashujaa 
Mkoani Shinyanga leo Jumanne Julai 25,2023.