Mkuu wa mkoa wa kusini pemba ameipongeza tcra kusogeza huduma kwa wananchi

Afisa Habari wa TCRA Judith Shao akitoa maelezo kuhusiana vitabu vya
Muongozo wa Mawasiliano Katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja
vya Gombani Mjini Pemba

Afisa Habari Mwandamizi wa TCRA Makao Makuu Mabel Masasi akimpa maelezo
mwananchi wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada Katika Viwanja vya
Gombani Mjini Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman akiweka alama ya vidole wa
ajili ya usajili laini ya simu katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika
Viwanja vya Gombani Mjini Pemba.
MKuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman akikabidhiwa kitabu cha
Muongozo wa Mawasiliano na Mkuu  wa Kanda ya Zanzibar wa  Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA)  Esuphatie Masinga (katikati) wakati wa
Kampeni ya a Mnada kwa Mnada wa TCRA katika Viwanja vya Gombani Mjini
Pemba.K kushoto ni Mkuu wa Kanda ya Mashariki TCRA Mhandisi Lawi Odiero
na watatu kutoka kushoto Afisa Habari Mwandamizi wa TCRA Makao Makuu
Mabel Masasi
Wananchi wakipata maelezo kuhusiana na usajili kwa alama za vidole
katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Viwanja vya Gombani Mjini Pemba.
TCRA kampeni ya Mnada kwa Mnada Nyehunge Wilayani Sengerema  katika utoaji wa Elimu ya Usajili wa laini
kwa kutumia alama za vidole.

Kampeni ya Mnada kwa Mnada imeanza 0ktoba 11 katika maeneo Kome Pamoja
Maisome kwa siku mbilimbili  ikiwa ni
kuwafikia wananchi wengi katika wilaya hiyo.
Akizungumza katika Kampeni ya  Mnada
kwa Mnada katika Viwanja vya Nyehunge Wilayani Sengerema Mkuu wa Kanda
Ziwa  Mhandisi Francis Mihayo amesema
wamejipanga kuwafikia wananchi wote wawemejisajili laini za simu kwa alama za
vidole.

Mhandisi Mihayo amesema katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa NIDA wapo katika kusajili wananchi vitambulisho kwa
ajili ya kufanya Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Wakazi wa Nyehunge Wilayani Sengerema na viunga vyake wamejitokeza kwa
wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada
ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu,
Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni 
na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili 
ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho
vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa
laini za simu.

Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 16 lengo kuu ni nchi nzima
kufiwa na Kampeni hiyo katika kuwawezesha wananchi kupata elimu ya Mawasiliano
Pamoja usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Amesema ni fursa kwa wananchi wa Sengerema kujitokeza kujisajili laini za
simu kwa alama za vidole na  huduma
nyinginezo  kutokana  na kuwepo kwa mnyororo   wadau wa 
mawasiliano.

Aidha Mihayo  amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa
ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za
vidole ili wasiweze kumuacha mtu yeyote kutotumia simu ifikapo Desemba 31 mwaka
huu.

Amesema muda uliopo ni miezi mitatu hivyo Wananchi wakamilishe taarifa
zinazohitajika katika kujisajili laini za simu 
kwa alama  za vidole ili kuondoa
usumbufu mwisho wa Desemba kwa watu kupanga foleni.

Mhandisi Mihayo amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika
mawasiliano ya simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.

Amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa
Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau
katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo
Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya
jinai ya matumizi ya simu.
Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha
kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia
kitambulisho cha taifa cha NIDA.

Mhandisi Mihayo amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi
ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

“TCRA tupo tayari 
kuwafikia  wananchi katika utoaji
wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika
huduma hiyo” amesema Mhandisi Mihayo.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio
umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za
simu kwa alama za vidole hali na kufanya wananchi wengi wamepata vitambulisho
vya Taifa na kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Masasi amesema  Wananchi wa watumie
Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu
husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.

Ameongeza kuwa watahakikisha kila mwananchi anajisajili kwa alama za vidole
kwani Watu wana haki ya kuwa na mawasiliano ya simu.