Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, ametoa tahadhari kwa wananchi
wa eneo la Ndembezi Mazinge Manispaa ya Shinyanga kutokana na uwepo wa
dalili za Volcano.
wa eneo la Ndembezi Mazinge Manispaa ya Shinyanga kutokana na uwepo wa
dalili za Volcano.
Akiongea na EATV & EA Radio leoTelack, amesema kuwa amewataka wakazi
wa eneo hilo lililopo Kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga,
kukaa mbali ili kuepuka kupata madhara endapo hali hiyo ikiwa sio ya
kawaida.
wa eneo hilo lililopo Kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga,
kukaa mbali ili kuepuka kupata madhara endapo hali hiyo ikiwa sio ya
kawaida.
‘Hili eneo linaonekana kama lava au Volcano, lakini hatujathibitisha
bado maana udongo unaotoka ni wa baridi, sasa isije kutokea udondo wa
moto ukaleta madhara’, ameeleza.
Aidha mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa, ‘Hili suala lipo kwa wiki ya
pili sasa na ni karibu kiasi na makazi ya watu lakini Watalaamu wa
Jiolojia walikuja na hawakubaini madhara yoyote lakini leo (Septemba 21,
2019), kuna watalaamu wanaingia wao ndio watatueleza zaidi’.
Kuhusu mazingira ya eneo, RC Telack amesema kuwa ni kilima ambacho sio
kikubwa sana lakini kimekuwa kikitoa udongo tepetepe, ambao unatoka
chini kupanda juu lakini kwa mujibu wa wazee wa zamani katika eneo hilo,
hicho kitu si cha kawaida kihistoria.