Mshitakiwa adai sehemu zake za siri zimetoweka kimaajabu baada ya kutembea na mtoto wa sheikh

Mshtakiwa
Faraji Ramadhani mwenye umri wa miaka 27 ameiomba Mahakama imruhusu
ajidhamini mwenyewe kutokana na sehemu zake za siri kutoweka hivyo
kupata maumivu makali anapokuwa Mahabusu.


“Hakimu
nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mtoto wa Shekhe, Ustadhi huyo
alinionya sana kuachana na Binti yake lakini sikusikia ndio chanzo cha
sehemu zangu za siri kupotea, nikiwa nyumbani natumia dawa za miti
shamha kutuliza maumivu”-Alisema

Kutokana
na malalamiko hayo Hakimu Manase aliamuru mtuhumiwa huyo aliyefikishwa
Mahakamani hapo kwa kosa la wizi wa Kompyuta akaguliwe na baada ya
askari kumkagua ilibainika anachokisema ni kweli.

Hata
hivyo Hakimu Diana Manase wa Mahakama hiyo ya Mwanzo Jijini Mbeya
aligoma kumruhusu kujidhamini kwa madai akitoroka hawezi kujua wapi kwa
kumpata na kumtaka avumilie kwakuwa tatizo kalitafuta mwenyewe maana
shekhe alimuonya aachane na Binti yake akakaidi, Kesi imeahirishwa hadi
September 27 mwaka huu.