Mvua
iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha jana jioni Mkoani Songwe
imesababisha uharibifu wa nyumba Zaidi ya 360 Katika Wilaya za Mbozi na
Momba pamoja na kujeruhi watoto wawili.

Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen Nicodemus Mwangela mapema leo ametoa
taarifa hiyo mara baada ya kukagua hali ya uharibifu wa makazi ya watu
na taasisi za serikali ambapo ameziagiza halmashauri husika kurejesha
miundombinu ya serikali iliyoharibika.

“Kuna wananchi wamepata madhara lakini wametibiwa na kurejea nyumbani,
nawapongeza sana viongozi na majirani ambao waliwahi kutoa msaada kwa
wahanga aidha ninaagiza halmashauri za Momba na Mbozi warekebishe haraka
nyumba za walimu na madarasa ili huduma ziendelee.”, amesema Brig. Jen.
Mwangela.

Aidha ametoa pole kwa wahanga na amewapongeza majirani wa waliopata
uharibifu wa nyumba kwa kuwahifadhi wenzao jana usiku huku akiwa
hakikishia kuwa Kamati za Usalama za Wilaya na wataalamu wanafanya
tathmini ya uharibifu na kupanga namna ya kutoa msaada.

Brig. Jen. Mwangela amewataka wananchi wote kuchukua tahadhari kwakuwa
mvua za Mkoani Songwe ni nyingi hivyo waimarishe makazi yao pia watoe
taarifa mapema endapo utatokea uharibifu wowote.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi Hanji Godigodi amesema wataalamu wa
Halmashauri wanaendelea na tathmini ya hali ya uharibifu na kuwa nyumba
za walimu na shule zitafanyiwa marekebisho haraka.

Afisa Mtendaji kata ya Msangano Halmashauri ya Wilaya ya Momba Focus
Kadule amesema baada ya tathmini ya hali ya uharibifu katika kata yake
ataitisha Mkutano wa hadhara ili wananchi waweze kujitolea kuwasaidia
waliopata uharibifu kutokana na mvua hizo.

Fadeli Ng’aala mkazi wa Kijiji cha Hamwelo Halmashauri ya Mbozi amesema
mvua iliyoambatana na upepo imeezua paa la nyumba yake huku yeye na
watoto wakiwa ndani na kusababisha uharibifu wa vyakula na vifaa vingine
kama vitanda, magodoro, televisheni, solar na masofa.

Naye Mwalimu Jacob Sambilila wa Shule ya Msingi Nkala Halmashauri ya
Wilaya ya Momba amesema mvua zilianza saa tisa mchana na kusababisha mti
kuangukia darasa hali iliyozua taharuki kwa wanafunzi lakini pia baada
ya kurudi nyumbani kwake alikuta nyumba anayoishi imeezuliwa.

“Baada ya kutoka kazini nilikuta nyumba ya mwalimu mwenzangu imeezuliwa
na nilipofika kwangu nimekuta nyumba imebomoka na kuezuliwa na
kusababisha uharibifu hata kwenye chakula chote nilichotunza
kimeharibika na vifaa vya ndani.”, amesema Mwalimu Sambilila.