Mwalimu katili aliyemvunja mgongo hosea apandishwa kizimbani

Mahakama ya Wilaya ya Njombe

Na Mwandishi Wetu, APC BLOG NJOMBE

Mwalimu Focus mbilinyi amefikishwa katika mahakama ya
Hakimu mkazi mkoa wa Njombe akikabiliwa na Tuhuma za kumsababishia
ulemavu mwanafunzi Hosea Manga anae daiwa kupigwa hadi kuvunjwa mgongo.

Shauri hilo namba 141 la mwaka 2019 linamkabili mwalimu huyo dhidi ya jamhuri kwa kumpiga mwanafunzi hadi kusababishia ulemavu.

Akisoma
shauri hilo mwendesha mashtaka wa serikali Elizabeth Malya amesema
mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo siku ya marchi 21,

2017  katika  shule ya msingi Madeke kwa kumning’iniza mtoto Hosea
Manga dirishani kwa mtindo wa miguu juu huku kichwa kikielekezwa chini
na baadae adhabu ya viboko kumi hali iliyompelekea kuanguka chini na
kuvunjika mgongo.

Mwendesha mashtaka ameeleza kuwa mwalimu
Mbilinyi aliitoa adhabu hiyo baada ya mtoto huyo kufeli maswali ya
hesabu kumi alizozitoa darasani .

Hosea ni miongoni mwa wanafunzi
sita wanaotajwa kuandibiwa siku hiyo na huku idadi ya viboko ikienda
sambamba na idadi ya hesabu walizokosa ambapo yeye alipatiwa adhabu hiyo
baada ya kukosa hesabu zote kumi.

Mara baada ya adhabu
alipelekwa zahanati ya kijiji cha madeke na ambako madaktari walishindwa
kumsaidia  na kuagiza akimbizwe kituo cha afya lupembe ambako nako
ilishindikana na baadae akafikishwa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe
kibena, kisha Hospitali ya ikonda ambako baada ya kupimwa pia alipewa
rufaa ya kupelekwa hospitali ya Taifa ya muhimbili ambapo baada ya
vipimo alibainika kuvunjika mgongo.

Mnamo tarehe 4 mwezi april
mwaka 2017 mtoto hosea aliruhusiwa kutoka Hospitali ya taifa ya
Muhimbili na kupewa baiskeli itakayomsaidia kutembea kutokan na kupooza
kwa eneo lote la mwili kuanzia maeneo ya kiunoni hadi miguuni.

Hosea
Manga alikumbwa na maswahibu hayo akiwa darasa la tatu mwaka 2017
ambapo hadi sasa alitakiwa kuwa darasa la tano akijiandaa kuingia darasa
la sita, lakini hawezi tena kuendelea na masomo kwa sasa kutokana na
kuhitaji uangalizi wa karibu akiwa na wazazi wake hususani suala la
usafi , kutoka na baadhi ya viungo vyake vya mwili kushindwa kufanya
kazi.

Hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Njombe
Irvan Msaki ameahirisha kesi hiyo na kutangaza kusikiliza tena nov 12
kutokana na kutokuwako kwa  mashahidi wa upande wa mshtakiwa.
  Mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana .