Mwenge wa uhuru waridhishwa na miradi 10 ya maendeleo halmashauri ya manispaa ya shinyanga

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Bwana Abdalla Shaim Kaim amepongeza juhudi zilizofanyika katika
ukamilishaji wa miradi ya maendeleo kwa kiwango chenye ubora katika Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga.

Ametoa pongezi hizo leo
Ijumaa Julai 28,2023 baada ya kutembelea na kuona miradi mbalimbali ya
Maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga baada ya kukamilisha mbio
zake Wilayani kishapu.

Kiongozi huyo wa Mbio za
Mwenge wa uhuru Taifa amekagua nyaraka zote na kujiridhisha kuwa miradi yote
kumi (10) imetekelezwa kwa kiwango na ubora huku akielekeza kuondolewa kwa
changamoto ndogo ndogo zilizobainika katika baadhi ya miradi ambapo amesisitiza
kukamilisha kwa wakati miradi ambayo bado inatekelezwa ili iweze kuwanufaisha
wananchi.


Mbio za Mwenge wa uhuru kwa Mwaka 2023 zimefika katika miradi yetu kwanza
kabisa tumepokea taarifa zinazohusiana na miradi baada ya kupokea taarifa
tumetembelea tumejionea tumekagua shughuli mbalimbali zinazohusiana na miradi
sambamba na kukagua nyaraka mbalimbali zinazohusiana na miradi hiyo”

“Upande
wa nyaraka zimepangwa vizuri na tumekagua tumejiridhisha pamoja na ukaguzi
ambao tumefanya kwa upande wa miradi viwango vimezingatiwa niseme hongereni
sana  kwa kazi nzuri mwenge wa uhuru
umeridhi”.
amesema Abdalla Kaim

Katika
Manispaa ya Shinyanga Mwenge wa uhuru  umekimbizwa umbali wa kilomita 72.5 ambapo umefungua
na kuweka mawe ya Msingi  kwenye miradi
kumi ya Maendeleo yenye zaidi ya Bilini mbili, ikiwa ni pamoja na kukagua hifadhi
ya mazingira,klabu ya wapinga rushwa na klabu 
ya lishe katika shule ya sekondari ya Rajani iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Kauli
mbiu ya mbio za mwenge kwa Mwaka huu inasema tunza mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na
uchumi wa Taifa.

Mkesha wa Mwenge wa
uhuru  utakuwa  katika eneo la uwanja wa saba saba Kambarage
mjini Shinyanga,utakaofanyika sanjari na shughuli nyingine ikiwemo upimaji afya
kwa hiyari,elimu ya uraia kwa jamii  juu
ya masuala mbali mbali pamoja na Burudani.

Awali
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akipokea Mwenge wa uhuru upande
wa kulia ni mkuu wa Wilaya ya Kishapu.