Polisi wadai kuua majambazi wanne kagera

Watu
wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wamefariki Dunia wakati
wakijibizana risasi na Jeshi la Polisi katika eneo la Pori la Ngazi
Saba, lililoko wilayani Biharamulo mkoani Kagera.Kwa
mujibu wa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi
Liberatus Sabas, amesema tukio hilo limetokea wakati Polisi wakiwa
katika Doria yao ya kawaida, ambapo waliona kundi la watu wakitokea
katika pori hilo na kuwaamuru kujisalimisha.

Kamanda Sabas amesema badala ya kutii amri, watu hao waliwarushia Polisi
risasi na polisi walipojibu walifanikiwa kuwapiga risasi na kupelekea
vifo hivyo.
Kamishna huyo amesema kuwa Polisi kwa sasa wanaendesha operesheni maalum
katika Mikoa ya Geita, Kigoma na Kagera, kufuatia mikoa hiyo kuwa na
matukio mengi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.