Naibu waziri masauni aagiza mkuu wa chuo cha polisi dar aondolewe na ashushwe cheo

Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amemtaka Inspekta Jenerali wa
Polisi (IGP) Simon Sirro kufanya mabadiliko ya uongozi kwenye Chuo cha
Polisi Dar es Salaam kutokana na kukiuka maagizo yake katika ujenzi wa
mabweni chuoni hapo.


Pia,
Masauni amemuelekeza IGP Sirro kumuondoa Mkuu wa Chuo hicho, Antony 
Ruttashuburugukwa na kumshusha cheo kutokana na kosa hilo.

Akizungumza
leo Jumatano Novemba 27, 2019 akiwa chuoni hapo, Masauni amesema
alielekeza katika ujenzi huo watumike wafungwa kufanya kazi za vibarua
ili kuokoa fedha lakini mkuu huyo wa chuo hakutekeleza agizo hilo.

“Rais
alikubali kutupatia Sh700 milioni kwa ajili ya ujenzi wa mabweni,
tuliangalia na kuona tunaweza kuokoa Sh210 milioni za kuwalipa vibarua
kwa kuwatumia wafungwa.”

“Nilizungumza
na kamishna wa magereza akasema hilo linawezekana hivyo nikamuelekeza
mkuu wa chuo kufanyia kazi suala hilo lakini leo nimekuja nakuta hali
hii hakuna wafungwa,” amesema Masauni

Wakati
Masauni anakagua ujenzi huo alikuta vijana wakifanya kazi na
alipowahoji walimuleza kuwa wao ni vibarua wanaolipwa kwa siku.