Naibu waziri wa madini asitisha utoaji wa leseni ya kuchimba dhahabu kwa mafahali wawili singida

Serikali
imeingilia kati mgogoro uliodumu kwa muda mrefu katika eneo la
wachimbaji wadogo lililopo katika Mlima wa Sakenke kata ya Misigiri
Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

Mgogoro
huo uliodumu kwa takribani miaka 3 ni kati ya mchimbaji mdogo aliyekuwa
afisa usalama  wa taifa mstaafu John Lutebeka, na Nabii Elia wote
wanagombea eneo hilo ambalo Lutebeka anamiliki ardhi ya juu na Elia
ameliombea Leseni ya Uchimbaji Madini.
Akizungumza
kwenye eneo linalogombewa, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo,
amewataka Lutebeka, Nabii Elia na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida,
Chone Malembo wafike ofisini kwake Jijini Dodoma siku ya Jumatano
Oktoba 16 mwaka huu kwa ajili ya kutatua mgogoro huo na kila mmoja aje
na vielelezo vinavyomruhusu kuchimba madini katika eneo hilo.
Aidha,
Nyongo amewataka Maafisa Madini kote Nchini kutoa elimu kwa wachimbaji
juu ya sheria za madini ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima maana kuna
haki ya umiliki wa ardhi ya juu na kuna haki ya umiliki wa ardhi ya
chini kwa maana ya leseni ya uchimbaji hawa wote wana haki sawa wanaweza
wakakaa wakazungumza  wakachimba pamoja.
Wakati
huo huo Naibu Waziri Nyongo, amemtaka Nabii Elia aachane na uchimbaji
wa madini karibu na nguzo za umeme anatakiwa awe mita 100 kutoka kwenye
nguzo za umeme, vinginevyo atachukuliwa hatua.
Pia
nyongo amewapongeza wachimbaji wa madini wa Mkoa wa Singida kwa ulipaji
mzuri wa kodi na amesema rasilimali ya madini ni ya Watanzania wote,
hatuko tayari kumuoneo mtu wala hatakubari mtu achimbe amdhulumu
mwingine.
“Kwenye
uchimbaji kuna kelele nyingi, kuna wengine wanamiliki leseni nyingi
hata kuzihudumia hawawezi, mpaka sasa tumefuta leseni elfu 13 hivyo wale
wanaojua wasitumie ujuaji wao kuwadhuru wengine tutampa haki mwenye
haki yake,” alisema Nyongo.
Awali
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Malembo, alisema kwa nyakati
tofauti, ofisi yake imesuluhisha  mgogoro huo, lakini Lutebeka huwa
haridhiki na maamuzi tunayofikia ikabidi tuligawe eneo hilo leye hekari
7.2 na kumpa Lutebeka hekari 4 lakini bado hakuridhika.
Akizungumza
kwa  masikitiko, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Huhahuka amesema anasikitika
kuingizwa kwenye mgogoro huo ambapo Afisa Usalama wa Taifa Mstaafu
Lutebeka amekuwa akimtuhumu kuwa anawadhamini hao wanaotaka kuchimba
eneo hilo.
Kwa
mujibu wa Afisa Madini Mkazi wa Singida, Malembo amesema, kati ya Julai
na Oktoba 11 mwaka huu, wamekusanya mapato ya zaidi ya shilingi 1.3
bilioni, Mapato hayo ni sawa na asilimia 271.94 ya lengo  kwa awamu ya
kwanza la kukusanya shilingi 500,000,000, na asilimia 90.65 ya lengo la
mwaka la kukusanya shilingi 1,500, 000,000/=.