Nic yaahidi kutoa sh.milioni 26 kwa shule ya sekondari jitegemee

 


Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Mhe.Dkt.Elirehema Doriye akipokelewa na
viongozi wa Shule ya Sekondari Jitegemee baada ya kiwasili katika
Sherehe za mahafali ya 27 ya kidato cha Sita yaliyofanyika kwenye ukumbi
wa shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi
Mkuu wa NIC Mhe.Dkt.Elirehema Doriye akisalimiana na baadhi ya viongozi
wa shule ya Sekondari Jitegemee baada ya kuwasili katika sherehe za
mahafali ya 27 ya kidato cha Sita yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule
hiyo leo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi
Mtendaji wa NIC Mhe.Dkt.Elirehema Doriye akisaini kitabu cha wageni
katika ofisi ya Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee baada ya kuwasili
katika sherehe za mahafali ya 27 ya kidato cha Sita yaliyofanyika kwenye
ukumbi wa shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam.Mkuu
wa Shule ya Sekondati Jitegemee Kanali Robert Kessy akizungumza mara
baada ya kuwasili Mkurugenzi Mtendaji wa NIC katika ofisi yake leo
kwaajili kuhudhulia sherehe za mahafali ya 27 ya kidato cha Sita
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi
Mtendaji wa NIC Mhe.Dkt.Elirehema Doriye (Wa kwanza kushoto)
akiongozana na baadhi ya viongozi wa shule ya Sekondari Jitegemee baada
ya kuwasili katika sherehe za mahafali ya 27 ya kidato cha Sita
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
Mtendaji wa NIC Mhe.Dkt.Elirehema Doriye akizungumza katika mahafali ya
27 ya kidato cha Sita yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule hiyo leo
Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya Sekondari Jitegemee Brigedia Jenerali
(Mstaafu) Lawrence Magere akizungumza katika mahafali ya 27 ya kidato
cha Sita yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule hiyo leo Jijini Dar es
Salaam.
Mkuu wa shule ya Sekondari Jitegemee Kanali Robert Kessy akizungumza
katika mahafali ya 27 ya kidato cha Sita yaliyofanyika kwenye ukumbi wa
shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam.Makamu
Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee Meja Mao Waryoba akizungumza
katika mahafali ya 27 ya kidato cha Sita yaliyofanyika kwenye ukumbi wa
shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Mhe.Dkt.Elirehema Doriye
akitoa vyeti kwa wahitimu waliofanya vizuri kwenye masomo yao katika
mahafali ya 27 ya kidato cha Sita yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa
shule ya sekondari Jitegemee Jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wahitimu wa kidato cha Sita shule ya Sekondari Jitegemee
akisoma risala katika mahafali ya 27 ya kidato cha Sita yaliyofanyika
kwenye ukumbi wa shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Scout wa shule ya Sekondari Jitegemee wakitoa burudani katika mahafali
ya 27 ya kidato cha sita yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule hiyo leo
Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Sekondari Jitegemee wakitoa burudani kwenye mahafali ya 27
ya kidato cha sita yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule hiyo leo Jijini
Dar es Salaam.

Wahitimu wa kidato cha sita wakiwa kwenye ukumbi wa mahafali ya 27 ya shule hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Wazazi
na walezi wa wahitimu wa kidato cha sita shule ya Sekondari Jitegemee
wakiwa kwenye ukumbi wa mahafali ya 27 ya shule hiyo leo Jijini Dar es
Salaam.

(PICHA NA EMMANUEL MBATILO)

NA EMMANUEL MBATILO

Shirika la Bima la Taifa (NIC)
limetoa kiasi cha shilingi Milioni 26 kwaajili ya ukarabati wa mabweni
ya shule ya sekondari Jitegemee ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada
zinazofanywa na shule hiyo.

Akizungumza katika Mahafali ya 27
ya kidato cha Sita shule ya Sekondari Jitegemee (JKT) leo Jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Mhe.Dkt.Elirehema Doriye amesema

Shirika la Bima la Taifa (NIC)
limetoa kiasi cha shilingi Milioni 26 kwaajili ya ukarabati wa mabweni
ya shule ya sekondari Jitegemee ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada
zinazofanywa na shuke hiyo.

Akizungumza katika Mahafali ya 27
ya kidato cha Sita shule ya Sekondari Jitegemee (JKT) leo Jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Mhe.Dkt.Elirehema Doriye amesema
menejimenti ya NIC imepokea wazo la menejimenti ya Shule ya Sekondari
Jitegemee la kuwa na ushirikiano hususani katika uelimishaji umma na
uwekazaji katika Bima.

“Ni kwa kweli niwaambie tu kuwa NIC
kama mdau mkubwa wa maendeleo nchini kwa kuongozwa na sera ya kurudisha
kwa jamii, mliomba kiasi cha shilingi Milioni 8, tunachangia Shilingi
Milioni 26 ambayo ni mara tatu ya mlioiomba”. Amesema Dkt.Doriye.

Aidha Dkt. Doriye amewataka
wahitimu kubadili maarifa yao kuwa ujuzi utakaowapa fursa za kutumia
rasilimali zinazotuzunguka kuzalisha mali na kukuza biashara.

Pamoja na hayo Dkt.Doriye amesema
kuwa wale watakaoshindwa kuendelea na masomo moja kwa moja,
wajishughulishe na shughuli rasmi za kuingiza mapato halali.

“Msibweteke kuamini kuwa ajira ni
zile za kuwa ofisini tu hapana, taifa linahitaji kila Mtanzania achape
kazi popote alipo. Hii itasaidia katika kuongeza tija na pato kwa mtu
mmoja mmoja na taifa hivyo huduma za kijamii kuimarika zaidi”. Amesema
Dkt.Doriye.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo
Kanali Robert Kessy amesema wamekuwa wakijitahidi kuwaeleza wazazi na
walezi wa wanafunzi kuhusu umuhimu wa ulipaji ada ingawa mpaka sasa
umekuwa hafifu na kupelekea wanafunzi kurudishwa nyumbani ili kuweza
kulipa ada hivyo kusababisha kukosa vipindi vya masomo darasani.

“Kuna wazazi bado wanakuja kuomba
uvumilivu kwasababu shule yetu ni yakusomesha watoto wote hasa maskini
huwa tunawasikiliza ila mrejesho wenu wazazi na walezi sio mzuri”.
Amesema Kanali Kessy.