Ofisa
msajili msaidizi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa Nida Mkoani
Shinyanga Haruna Mushi, pamoja na wakala wa usajili laini za simu za
mkononi Victor Isack Vicent, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa
tuhuma za kutoza fedha wananchi kiasi cha Shilingi 30,000, ili wawapatie
namba za Nida na kusajili laini zao za simu kwa alama za vidole.
Tukio
hilo limetokea leo Jumatatu Januari 20,2020 majira ya saa saba mchana
wakati mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alipofika kwenye
ofisi za mamlaka ya vitambulisho vya taifa Nida Mjini Shinyanga baada ya
kupata taarifa za wananchi kuombwa fedha ili wapate namba za Nida.
Akielezea
tukio hilo mkuu huyo wa wilaya Mboneko, ambaye pia ni mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Shinyanga ,alisema wakati akiwa
kwenye ofisi hizo za Nida, amepata taarifa za wananchi kuombwa pesa
kutoka kwa wakala wa usajili la laini za simu za mkononi ambaye alikuwa
akifanya mawasiliano na ofisa huyo wa Nida.
Alisema
mara baada ya kumkamata wakala huyo wa usajili wa laini za simu za
mkononi kwa alama ya vidole, walipomfikisha Polisi na kuanza kumhoji
kwanini anatoza fedha wananchi ili awapatie namba za Nida, na wakati
yeye siyo mtumishi wa Nida, ndipo akasema huwa anashirikiana na mmoja wa
maofisa na Nida.
“Baada
ya kumkamata wakala huyu wa usajili wa laini za simu za mkononi kwa
alama za vidole, ndipo akamtaja Ofisa huyu wa Nida Haruna Mushi kuwa
wanashirikiana naye kuomba fedha wananchi, ambapo yeye ndiyo mtoaji wa
namba za Nida, na wakala huyu wa simu ndiyo mkusanyaji wa fedha,”alisema
Mboneko.
“Tulipopewa
taarifa hiyo ikabidi tumkamate na huyu Ofisa wa Nida Haruna Mushi,
ambapo tumefanya uchunguzi wa simu zao na kubaini kuwepo na mawasiliano
ya wananchi kuwaomba fedha na baadhi yao wameshatuma fedha hizo kwenye
simu zao, ambapo bado tunaendelea na uchunguzi zaidi,”aliongeza.
Pia
alitoa wito kwa wananchi wa Shinyanga kuacha tabia ya kutoa fedha ili
kupata namba za vitambulisho hivyo vya taifa Nida kwani Serikali inatoa
namba hizo bure, huku akiagiza maofisa wa Nida wafanye kazi usiku kucha
na kutofunga ofisi hizo, hadi pale watakapo wamaliza watu wote kuwapatia
namba hizo za Nida.
Kwa
upande wakala huyo wa usajili wa laini za simu za mkononi kwa alama ya
vidole Victor Isack Vicent, alikiri kufanya kazi hiyo ya kuomba fedha
wananchi ili awasaidie kupata namba za Nida, kwa kushirikiana na ofisa
huyo wa Nida Bwana Haruna Mushi, huku akiomba msamaha kwa kufanya makosa
hayo.
Hata
hivyo Ofisa huyo msajili msaidizi wa Nida mkoa wa Shinyanga Haruna
Mushi, alikanusha tuhuma hizo za kushirikiana na wakala huyo wa usajili
wa laini za simu za mkononi kwa alama ya vidole kuomba fedha wananchi,
huku akikiri huwa anampatia majina ya watu kwa SMS na kisha
kumuangalizia namba za Nida.
Kaimu
kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Joseph Paulo, alisema kuwa
upelelezi bado unaendelea ambapo wamewakabidhi Takukuru na ukikamilika
watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Ofisa msajili msaidizi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa Nida mkoani
Shinyanga Haruna Mushi (kushoto) akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa
tuhuma za kutoza fedha wananchi Shilingi 30,000 ili awapatie namba za
Nida akishirikiana na wakala wa usajili wa laini za simu kwa alama ya
vidole Victor Isack Vicent.Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Ofisa
msajili msaidizi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa Nida mkoani
Shinyanga Haruna Mushi (kushoto) akiwa kwenye kituo cha Polisi wilaya ya
Shinyanga kwa tuhuma za kutoza fedha wananchi Shilingi 30,000 ili
awapatie namba za Nida akishirikiana na wakala wa usajili wa laini za
simu kwa alama ya vidole Victor Isack Vicent (kulia)
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akitoa tahadhari kwa wananchi
kuacha tabia ya kutoa fedha ili wapatiwe namba za vitambulisho vya taifa
Nida, ikiwa namba hizo zinatolewa bure.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwataka wananchi wawe na
uvumilivu na kuacha kutoa fedha ili kupata namba za Nida, ikiwa zoezi
hilo litaendelea licha ya laini kuzimwa ili wananchi wote wapate namba
za Nida na kusajili laini zao kwa alama ya vidole.
Wananchi
wakiwa kwenye ofisi za Nida Shinyanga mjini wakimsikiliza mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko na kutakiwa kutotoa fedha yoyote ile
ili wapate namba za Nida.
Wananchi
wakiwa kwenye ofisi za Nida Shinyanga mjini wakimsikiliza mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko na kutakiwa kutotoa fedha yoyote ile
ili wapate namba za Nida.
Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog