Egidia vedasto
Arusha.
Ametoa ufafanuzi huo kwenye mkutano wake na asasi zisizo za kiraia Jijini Arusha baada ya Wasamaria wema kutoka Asasi mbalimbali kutoa malalamiko yao juu ya vikwazo ambavyo wamekuwa wakikumbana navyo katika kesi hizo na kukatishwa tamaa kwa majibu na kauli mbaya kutoka kwa baadhi ya viongozi wa serikali.
Aidha Makonda amesisitiza Asasi hizo kuwa na ushirikiano na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Serikali kwa ujumla hususan katika suala la Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Arusha.
“Nawakumbusha kuwa na tabia ya kuchangia katika huduma mbalimbali kama kukamilisha vifaa katika Maabara Shuleni, lakini pia katika zoezi la kufunga kamera na taa barabarani mji mzima, hatua itakayo wapa mazingira rafiki Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika majukumu yao” Amesema Makonda.
Hatahivyo amependekeza kuundwa kwa Kamati ndogo itakayochunguza mkinzano wa sheria zinazokwamisha utendaji katika majukumu sambamba na kukusanya taarifa za idadi ya watu wote wenye ulemavu na mahitaji yao kwa Mkoa mzima.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Uchumi katika Halmashauri ya Wanawake wa Kifugaji (PWC) Timothy Ole Yaile amepongeza kufanyika kwa mkutano huu mhimu utakaotupa nafasi ya kueleza changamoto tunazopotia katika Taasisi zetu ili zitatuliwe.
Hatahivyo amebainisha matarajio yake kutokana na mikutano kama hii iwapo itaendelea, kwamba watabadilishana mawazo na kupatiwa majibu kwa yale yanayowatatiza kama Taasisi.
“Kipekee nimefurahishwa na utatatibu huu wa kutuita sisi Asasi za Kiraia na kukaa pamoja, haijawahi kutokea zaidi tunatafutwagwa ili kuchangia pesa na vitu vingine, napendekeza hii iwe muendelezo” Ameeleza Olpe Yaile.
Ole yaile ametaja majukumu yanayofanywa na Taasisi ya (PWC) inajikita katika kuwasomesha watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu na wale wanaoishi katika famillia zisijali kuhusu elimu, ambapo hadi sasa zaidi ya wasichana 900 wamenufaika, 700 tayari wamemaliza masomo na 200 bado wako shule, kuchimba visima na kuhamasisha uoteshaji wa majani ya kulisha mifugo.
Pia mesema, Wanatoa elimu kwa vikundi vya wanawake kwa kuweka na kukopa, visivyopungua 700, na kuwapa elimu juu ya masuala ya ukatili na kuzijua haki zao kuanzia ngazi za kijamii, kiuchumi na kisiasa.
“Pamoja na shughuli zote tunazozifanya pia tunahamasisha uhifadhi na utunzaji wa mazingira ikiwemo kulinda vyanzo vya maji na kupanda miti katika Wilaya tatu za mradi ambazo ni Ngorongoro, Monduli na Longido” ameongeza Ole Yaile.