Mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa mwatara wazinduliwa

NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mtwara
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezindua
Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Mtwara (MIG) katika Kongamano la Uwekezaji na
Maonyesho ya Biashara lililofanyika kwenye viwanja vya Chuo Cha Ualimu Mtwara.
Mwongozo
huo umetayarishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa
kushirikiana na Mkoa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP).
“Kuja
kwenu Mtwara leo hii hamjapoteza nauli na muda wenu, mmekuja Mtwara mahali
sahihi kwa uwekezaji na mtatumia nafasi ya leo kusikia nini kimeandaliwa kwa
ajili ya kuwaambia fursa zipi zinapatikana mkoani Mtwara.” Amesema Waziri Mkuu
Majaliwa
Waziri
Mkuu amesema Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuiondoa Tanzania
kwenye uchumi wa chini kwenda Uchumi wa Kati na hakuna njia nyingine isipokuwa
ni kuvutia uwekezaji, Serikali inakaribisha wawekezaji kuwekeza hapa nchini iwe
ni Mtanzania au mgeni kutoka nje ya nchi atapokelewa ili aweze kuwekeza hapa
nchini.
“Wakati
nikizungumza na wakuu wa mikoa Juni 18, 2018 jijini Dodoma nilitoa maelekezo na
dira ya kila mkoa kupata wawekezaji, niliagiza kila mkoa lazima ujipange
kuhakikisha unatangaza fursa zilizopo katika mkoa.”

Alifafanua Waziri Mkuu.

Mheshimiwa
Majaliwa alisisitiza Mikoa ambayo bado haijaandaa miongozo ya uwekezaji ifanye
hivyo mara moja kabla mwaka huu haujaisha. Pia aliwaonya watumishi wanaokuwa
vikwazo kwa wawekezaji waache mara moja na wanaobainika wachukuliwe hatua
stahiki.
“Niipongeze
Taasisi ya ESRF chini ya Mkurugenzi wake Dkt. Tausi Kida imefanya kazi kubwa na
nzuri, baada ya kufanya utafiti imetoa tathmini ya nini kifanyike, wapi tufanye
nini ili tuweze kufanikisha uwekezaji hapa nchini” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa
na kuongeza….Kila ninapokwenda kuzindua Miongozo ya Uwekezaji nimekuwa
nikukutana na ESRF ikiongozwa na Dkt. Tausi Kida, hongera sana kwa kazi nzuri
mnayofanya.” Alipongeza Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu pia ameipongeza UNDP kwa kufanya kazi kwa pamoja na Serikali na kuahidi
kuwa Serikali itaunga mkono shughuli za UNDP ambazo Serikali ya awamu ya Tano
na zile zilizotangulia daima zimekuwa zikifanya kazi kwa pamoja na UNDP na
zinatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hii ya kimataifa.

Uzinduzi
huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki. Wakati akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia,
Mhe. Kairuki alieleza hatua ambazo Serikali imechukua kuboresha mazingira ya
uwekezaji nchini na kupelekea Tanzania kupanda kutoka nafasi ya 144 hadi 141
kwenye urahisi wa kufanya biashara duniani.
Mawaziri
wengine waliohudguria na kutoa neno ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.
Innocent Bashungwa, na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga.
Wakati
akitoa salaamu, Mwenyeji wa Mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa
aliwakaribisha wageni waalikwa na kuelezea jinsi Mkoa ulivyojipanga kuwapokea
na kuwasaidia wawekezaji. Pia alitoa fursa kwa Wakuu wa Mikoa jirani
walihudhuria halfla hiyo ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mtwara
kutoa neno. Waliohudhuria ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi, Mkuu wa
Mkoa wa Ruvuma Mhe. Chrintina Mdema na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi 
Evarist Ndikilo.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bi.Christine Musisi
alisema UNDP itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha maisha
ya wananchi. Alisema UNDP itaendelea kusaidiana na Mikoa katika utekelezaji wa
miongozo hii kwa kutoa ushauri wa kitaalam na rasilimali fedha panapohitajika.

Awali
akiwasilisha Muhtasari wa Fursa za Uwekezaji katika Mkoa wa Mtwara katika
Kongamano la Uwekezaji, Mtafiti Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya Utafiti wa
Uchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Oswald Mashindano alisema ESRF ilifanya utafiti
kwenye halmashauri zote za Mkoa wa Mtwara na utafiti huo ulibaini uwepo wa
fursa nyingi za uwekezaji. Dkt. Mashindano alitaja timu ya wataalam kutoka ESRF
walioshiriki kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji ikijumuisha Prof. Haidari Amani, Bi.
Margareth Nzuki, Bw. Mussa Mayala Martine, na Bw. James Kasindi.
Dkt.
Mashindano alitaja fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo zimepewa kipaumbele na
mkoa. Fursa hizi ziko katika makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwekezaaji
katika kilimo hasa korosho, kilimo cha umwagiliaji wa mpunga na miwa, ujenzi wa
miundombinu ya umwagiliaji wa mpunga na mazao ya bustani; uwekezaji katika
mifugo hasa ranchi na unenepeshaji wa mifugo; uwekezaji katika uvuvi hasa uvuvi
ndani ya bahari kwa kutumia nyenzo na teknolojia za kisasa pamoja na ufugaji wa
samaki; uwekezaji katika viwanda hasa Kuchakata Korosho na mazao mengine kama
mhogo, nazi, choroko, mbogamboga na matnda, kuchakata na kufungasha chimvi,
Chakula cha Mifugo, Kuchakata Samaki, Kiwanda cha Kutengeneza Maji ya Chupa nk.

Fursa
za uwekezaji katika eneo la miundombinu zilijumuisha ujenzi wa jengo kwa ajili
ya matengenezo na maegesho ya ndege, stendi za kisasa, ujenzi wa kituo cha
michezo ikijumuisha uwanja wa mpira, masoko ya kisasa nk. Aidha Dkt. Mashindano
alitaja makundi mengine ya fursa za uwekezaji kuwa ni pamoja na uwekezaji
katika utalii akilenga uwekezaji kwenye fukwe, michezo ya baharini, ujenzi wa
hoteli, majumba ya starehe, kambi za watalii, kuendeleza maeneo ya kihistoria
nk. Pia zilibainishwa fursa za uwekezaji katika huduma za kijamii zikijumuisha
afya na elimu. Kwa upande wa afya kuna fursa ya ujenzi wa hospitali na kiwanda
cha kutengeneza maji ya wagonjwa na vifaa tiba. Kwa upande wa elimu alitaha
fursa ya kuendesha chuo maalum cha ujuzi pamoja na shule binafsi za kisasa.
Baada
ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji washiriki walipata fursa ya kutembelea
maeneo mbalimbali ya uwekezaji Mkoani Mtwara.

Maonesho ya biashara na Uwekezaji yanafikia kilele leo Novemba 3, 2019.
 Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (watatu kushoto), akikata utepe, kuzindua
Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara (MIG), kwenye Chuo Cha Ualimu
Mtwara Novemba 1, 2019. Wanaoshuhudia ni kutoka kulia ni Waziri wa
Kilimo Mhe. Japhet Hasunga, 
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki  Mwakilishi Mkazi
wa UNDP, Bi. Christine Msisi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.
Gelasius Byakanwa. 
 Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (katikati), akionyesha nakala za Mwongozo wa
Uwekezaji Mkoani Mtwara (MIG), baada ya kuuzindua kwenye Chuo Cha Ualimu
Mtwara Novemba 1, 2019. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki (wapili kulia), Mwakilishi Mkazi
wa UNDP, Bi. Christine Msisi (wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
Mhe.Gelasius Byakanwa (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF,
Dkt. Tausi Kida. 
 Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, huku Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki (katikati)
akishuhudia, mara baada ya Waziri Mkuu kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji
Mkoa wa Mtwara Novemba 1, 2019.

Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, huku Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki (katikati)
akishuhudia, mara baada ya Waziri Mkuu kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji
Mkoa wa Mtwara Novemba 1, 2019.

 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia kongamano hilo na kisha kuzindua Mwongozo huo Novemba 1, 2019.
 Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji
Mkoa wa Mtwara (MIG) Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bi. Christine
Msisi akitoa hotuba yake.
 Viongozi waandamizi wa ESRF walioshiriki katika utafiti huo kutoka kushoto,Bw. Mussa Mayala Martine,  Dkt. Oswald Mashindano na Bi.
Margareth Nzuki.
 Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji
Mkoa wa Mtwara (MIG), Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga huku Mhe.
Kairuki (katikati) akishuhudia. 
 Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji
Mkoa wa Mtwara (MIG), Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent
Bashungwa huku Mhe. Kairuki (katikati) akishuhudia. 
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji
Mkoa wa Mtwara (MIG) Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bi. Christine
Msisi. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Uwekezaji), Mhe. Angela Kairuki (wapili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida. Mwongozo
huo umetayarishwa na (ESRF) kwa
kushirikiana na Mkoa wa Mtwara chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP).