Pentekoste arumeru wakabidhi vifaa vya afya vya mil9

Na Woinde Shizza ,ARUMERU
Kanisa
la Pentecoste Ngulelo linaloongozwa na Mwalimu Onesmo Nnko limekabidhi
vifaa vya afya vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9 kwa Mkuu wa
wilaya ya Arumeru Jerry Muro ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano
baina ya kanisa na Serikali.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo ambavyo vimetolewa kutokona na sadaka
za waumini wa kanisa la Pentecoste Arusha Jana , kiongozi wa kanisa hilo
mwalimu Onesmo Nnko amesema wao kama kanisa wana kila sababu ya
kuungana na serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za
afya ili kutengeneza jamii bora 
Alisema
kuwa kanisa lao limekuwa likitoa misaada mbalimbali katika sekta
mbalimbali ikiwemo ya elimu ,misaada kwa watu mbalimbali na kipindi
hichi wameamua kutoa katika sekta ya afya na wameanza na kituo Cha Afya
Cha Usa river  na wanampango wakiendelea kutoa msaada katika vituo
vingine vya afya vilivyopo katika mkoa huu.
“Nimeguswa
kutoa katika jamii na ndio maana nikawaamasisha waumini watoe ili
kutimiza maono nilionyeshwa na mungu,na tukumbuke kwamba ata katika
mistari ya biblia imeandikwa nibora kutoa kuliko kupokea ,hivyo napenda
kiwasihi wananchi wapende kutoa kuliko kupokea ,tusitoe kwa vile tunacho
bali tutoe ili tukapokee zaidi,na jinsi tunavyotoa ndivyo mungu
anatukumbuka katika mahitaji yetu “alisema Onesmo
Aliwataka
viongozi wengine wa dini  kuendelea kushirikiana na serikali katika 
maswala mbalimbali kwani serikali na kanisa ni mikono miwili ya kusaidia
jamii.
Akipokea
misaada hiyo Mkuu wa wilaya ya Arumeru  Jerry Muro amesema

kupatikana
kwa vifaa hivyo kutasaidia kuimarisha huduma pamoja na kuondoa
changamoto ya uhaba wa vifaa vya kutolea huduma 

“Kweli
vifaa hivi vitatusaidia kwani tulikuwa na uhaba wa baadhi ya vitu
katika kituo hichi Cha Afya  ,hivyo hivi vilivyotolewa vitatusaidia sana
napenda nikushukuru mwalimu Onesmo pamoja na waumini wako kwa kuamua
kujitoa  kwa ajili ya kutununulia baadhi ya  vifaa tiba kwa ajili ya
kituo chetu Cha Afya niwaombe viongozi wengine wa dini muige mfano
huu”alibainisha Muro
Akitoa
taarifa ya utoaji wa huduma za afya katika Halmashauri, mganga mkuu wa
wilaya Dkt. Maneno focus amesema kwa sasa huduma za afya zinazidi
kuimarika na wameamua misaada hiyo itolewa katika kituo cha afya cha usa
river ambacho Mhe Rais Magufuli alitoa shilingi milioni 500 kwa ajili
ya ujenzi ambao ulishakamilika na kituo kinatoa huduma za kisasa 
Mmoja
ya mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la  Edna  Ulomi  alishukuru
serikali kwa kiwasogezea huduma na kubainisha kuwa awali walikuwa
wakipata tabu kwenda kupata huduma katika hospital ya wilaya ya
patandi,aliongeza kuwa wauguzi wamekuwa wakiwapatia huduma Bora na nzuri
kuliko vituo vingine .
Vifaa
vilivyotolewa na kanisa Hilo la Pentecoste Arusha ni pamoja na mashine
ya kusafishia njia ya hewa kwa watoto wa changa (sunction
machine),vitanda 6 ,mashika 100,deliver set 3,matress for neonatial
unit,oxgen cycliner eflow meter 1, Mercury Bp machine 3, hospital screen
1,Bigstetcher 1,pamoja na Exmination bed 2.
Picha
ikionyesha mchungaji wa kanisa la Pentecoste Arusha mwalimu Onesmo Nnko
wa Kwanza kulia akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro
mashine ya kusafishia njia ya hewa kwa watoto wachanga Kama ishara ya
kukabidhi misaada yote walioitoa kwa kituo Cha Afya USA River