Picha: maonyesho ya ndege za kivita yalivyoibua shangwe sherehe za miaka 58 ya uhuru jijini mwanza

Moja
ya mambo yaliyovutia na kushangiliwa sana na wananchi kwenye sherehe za
Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara jana na miaka 57 ya Jamhuri, ni
miondoko ya ndege vita na onesho la makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wakishuka kwenye Helkpta za Kijeshi.


Sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza, zilipambwa na nyimbo, ngoma za jadi na
idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kutoka Mkoa wa Mwanza na mikoa
mingine nchini.


Kama
mchezo wa kwenye filamu, maonyesho ya ndege  za kivita yalianza kwa
ndege tatu kupita kwa kasi juu ya anga na kuibua shangwe kutoka kwa
viongozi na wananchi waliokuwa  uwanja wa CCM Kirumba

Kasheshe
likaja baada ya ndege za kivita zenye miungurumo ya vishindo zilipoanza
kukatiza angani na kuzua hofu kwa baadhi ya wananchi  waliojikuta
wakishindwa kuhimili vishindo hivyo na kuzimia kwa hofu. Baadae
lilifuata zoezi la Makomandoo wa JWTZ Kushuka Kwenye Helkopta za Kijeshi
kwa kutumia Kamba

VIDEO: Ndege
za kivita kadhalika ndege ya heshima zikipita mbele ya Rais na Amiri
Jeshi Mkuu, Dk John Magufuli wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru
na miaka 57 ya Jamhuri kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. #SherehezaUhuru58 pic.twitter.com/x4vc2rrrKO
— MPEKUZI (@mpekuzihuru) December 9, 2019